Home LOCAL PROF. MAKUBI AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA KUFUATA MIONGOZO YA UNUNUZI

PROF. MAKUBI AWATAKA WATUMISHI WA WIZARA KUFUATA MIONGOZO YA UNUNUZI


Na: Catherine Sungura,WAF-Dodoma

Wakurugenzi wa taasisi na wa Hospitali za rufaa za mikoa wametakiwa kufuata miongozo na sheria za manunuzi ili kuondoa hati chafu na zenye mashaka kwenye taasisi zao.
 

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya afya Prof. Abel Makubi wakati akiendesha mkutano wa baraza kuu la wafanyakazi wa Wizara ya afya lililofanyika jijini Dodoma.
 

Prof. Makubi amesema ni viongozi wanatakiwa kuwa mfano katika utekelezaji wa majukumu yao mahali pa kazi kwa kufuata miongozo na sheria ya manunuzi ya bidhaa kwa ajili ya mahitaji ya ofisi au ujenzi pamoja na maboresho ya miundombinu ya hospitali zao ili   kuondokana na hati chafu au zenye mashaka.

Aidha, Prof. Makubi aliwataka waganga wafawidhi wa hospitali za Rufaa za Mikoa  kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba kwenye hospitali zao.
 

“Ifike muda kila mgonjwa anayefika kwenye hospitali yako uhakikishe anapata dawa zilizopo kwenye mwongozo wa dawa (STG). Tunataka malalamiko yanayotolewa na wananchi yapungue ikiwemo ukosefu wa dawa pamoja na kutopata huduma kwa wakati”. Alisisitiza Prof. Makubi.
 

Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo aliwakumbusha viongozi hao pindi wanaporudi kwenye vituo vyao vya kazi kuwakumbusha madaktari walio chini yao kuandika dawa zilizopo kwenye muongozo huo na wahakikishe dawa wanazoziagiza ni zile ambazo zipo kwenye muongozo.
 

Prof. Makubi amewataka watumishi hao kutofanya kazi kwa mazoea na wanatakiwa kufanya kazi kulingana na kasi ya utendaji wa viongozi waliopo na kutekeleza majukumu wanayopangiwa kwa weledi.

Previous articleIGP SIRRO AWAGIZA MAKAMANDA KUFANYA OPERESHENI MWEZI MMOJA BARABARANI
Next articleWAZIRI DKT.NDUMBARO AKABIDHI VYETI YA UWEKEZAJI MAHI KWA KAMPUNI YA GRUMETI NA MWIBA HOLDINGS LTD, ATOA NENO KWA WAWEKEZAJI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here