MWANDISHI WETU
MWENYEKITI wa kamati ya Usajili ya Yanga, Hersi Said amesema hakuna mchezaji atakayezibiwa riziki kama atatakiwa na timu ya nje au klabu nyingine ya ndani ilimradi taratibu zifuatwe..
“Hatuwezi kuwabania wachezaji hata kidogo. Yeyote atakayepata nafasi ya kutoka tutamuachia atoke akajaribu maisha kwingine. Mpira sikuhizi ni zaidi ya ajira..
“Tulimuuza Kisinda kwa kuvuna dola 150,000 kupitia mauzo ya mchezaji mmoja tuliwanunua mastaa watatu Djuma Shabani, Fiston Mayele, na Jesus Moloko wote wanafanya vizuri.