Home LOCAL HABARI PICHA: WAOMBOLEZAJI DAR WAKIAGA MWILI WA PROF. NGOWI, DEREVA WAKE

HABARI PICHA: WAOMBOLEZAJI DAR WAKIAGA MWILI WA PROF. NGOWI, DEREVA WAKE


Viongozi mbalimbali wa Chuo Kikuu Mzumbe wakitoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Mhadhili wa Chuo hicho Profesa Prosper Honest Ngowi pamoja na Dereva wake Innocent Mringo waliopata ajali Mlandizi Mkoani Pwani Machi 28, 2022.



Wadau mbalimbali wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa miili ya Marehemu hafla iliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mtoto wa Marehemu wa Profesa Ngowi, Nana Ngowi (katikati) akitoa neno la shukrani kwa wadau na waombolezaji waliofika katika hafla ya kuuaga mwili wa Baba yao mpendwa Profesa Prosper Ngowi iliyofanyika leo Machi 31,2022 katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Hellen Ottaru Mwana zuoni lkutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe akitoa salamu za rambirambi akielezea Farsafa za Profesa Ngowi zilizolenga kubadilisha mitazamo ya wasomi na wananchi wa kawaida katika maisha.
Msanifu majengo kutoka Bodi ya Makandarasi Tanzania Mhandisi Neema Fuime akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Bodi hiyo iliyofanyakazi kwa ukaribu a Profesa Ngowi hukuakieleza mchango mkubwa alioutoa katika kuboresha mafunzo kwa makandarasi hapa nchini.
 

Mjumbe wa Bodi Benki ya Equity Profesa Ahmmed Amme akitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mjumbe mwenzao wa Bodi ya Benki hiyo Profesa Ngowi wakati wa hafla ya kuaga miili ya Profesa Ngowi na Dereva wake Innocent Mringo katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Profesa Kitila Mkumbo akitoa salamu zake za rambirambi akielezea wasifu wa Marehemu Profesa Honest Ngowi kwa kazi alizofanya wakati wa uhai wake

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS) Francis Kiwanga akitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Profesa Honest Ngowi aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya Taasisi hiyo, ambapo ameelezea umahiri wa Profesa huyo katika kutekeleza majukumu yake.

Wanazuoni wa Chuo Kikuu Mzumbe wakifuatilia kwa karibu Salamu mbalimbali zilizokuwa zikitolewa viwanjani hapo.
Wanafamilia ya Profesa Honest Ngowi wakiwa katika hafla hiyo wakifuatilia Salamu mbalimbali za rambirambi zilizokuwa zikitolewa viwanjani hapo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS) Francis Kiwanga akitia saini katika kitabu cha maombolezo mara baada ya kutoa salamu zake za rambirambi katika hafra hiyo.


PICHA NA: HUGHES DUGILO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here