Home LOCAL NDUGU ABDULRAHMAN KINANA ATEULIWA KUGOMBEA UMAKAMU MWENYEKITI CCM, MEMBE AREJESHEWA UANACHAMA

NDUGU ABDULRAHMAN KINANA ATEULIWA KUGOMBEA UMAKAMU MWENYEKITI CCM, MEMBE AREJESHEWA UANACHAMA

 

Dodoma, 31.3.2022

Kikao cha halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi kimemteua Abdrahman Kinana kuwa mgombea wa kiti cha makamu mwenyekiti wa CCM , Bara.

Kinana anachukua nafasi iliyoachwa wazi na mzee Philip Mangula ambaye ameandika barua ya kung’atuka nafasi hiyo na kuipeleka kwa mwenyekiti wa CCM rais Samia Suluhu Hassan.


Mzee Mangula ambaye leo ametimiza miaka 81 ya kuzaliwa anatajwa kuwa sehemu kubwa ya uhai wake amekuwa mtumishi wa serikali na Chama.

Amewahi kuwa Mkuu wa wilaya kisha mkuu wa mkoa na baadaye kuwa katibu mkuu wa chama cha mapinduzi kwa muda mrefu na baadaye kuchagukiwa kuwa makamu mwenyekiti wa CCM bara.


Katika mkutano wake na waandishi wa habari katibu wa NEC itikadi na uenezi Shaka Hamudu Shaka amesema jina la Kinana litapelekwa kesho kwenye mkutano mkuu maalumu wa taifa wa CCM ambao itafanya iteuzi wa mwisho wa jina hilo.

Pia amesema maandalizi ya mkutano mkuu huo maalumu yamekamilika na kwamba Mwenyekiti wa CCM ametembelea leo ukumbi huo na kuridhishwa na maandalizi yake.

Katiba ya CCM ibara ya 100 toleo la mwaka 2020, Makamu mwenyekiti wa CCM inasema atachaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa.
Aidha mwenyekiti wa CCM Rais Samia amempongeza Mangula kwa utumishi wake uliotukuka katika CCM kwa muda mrefu.

Pia NEC, imemrejeshea uanachama wake wa CCM aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje Benard Membe.

Previous articleHABARI PICHA: WAOMBOLEZAJI DAR WAKIAGA MWILI WA PROF. NGOWI, DEREVA WAKE
Next articleMWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM,RAIS WA TANZANIA MHE.SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU PAMOJA NA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA JIJINI DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here