NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Samia Suluhu imetoa bilioni 2 na milioni 450 kwa wizara ya maliasili na utalii kupitia mpango waustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 kwaajili ya kuboresha makumbusho zote saba zilizopo nchini na kuzifanya ziwe za kisasa.
Hayo yameelezwa na Dkt Noel Luoga mkurugenzi mkuu wa makumbusho ya taifa nchini katika maadhimisho ya miaka 55 ya Azimio la Arusha ambapo alisema kuwa Wana miradi takribani 15 ambayo itaenda kutekeleza kupitia fedha hizo katika makumbusho hayo kutokana na kuonekana ni ya zamani sana.
“Ni dhairi maonesho yaliyopo katika makumbusho yetu kama mnavyoyaona ni ya zamani sana tunahitaji kuyaweka yawe ya kisasa ili kuweza kuvutoa jamii na tunajivunia sana kupata fursa hii ya kuboresha makumbusho,” Alisema Dkt Luoga
Alifafanua kuwa kihistoria makumbusho zimekuwa zikifanywa programu nyingi za kielimu katika vituo vyake vyote ikiwemo uelimishaji jamii, utangazaji na wamejiwekea mikakati ya miaka mitano 2021/2026 ya kuwa na mpango wa masoko ambao ni mpango wa kwanza na hasa wanalenga kusimamia vyema katika utangazaji ili kufungua utalii zaidi katika makumbusho.
Kwa upande wake mkurugenzi wa makumbusho ya Azimio la Arusha Dkt Gwakisa Kamatula alisema kuwa mpaka kufikia miaka 55 ya kuzaliwa Azimio la Arusha wamejitahidi kuhifadhia historia ambayo imekuwepo toka kipindi cha nyuma hasa baada ya uhuru ambapo bado kuna jalada ambalo limetunza kumbukumbu halisi za maadhimio yalifanyika kipindi hicho Cha mwaka 1997.
Alisema wamejipanga kuzifanya makumbusho ziweze kuhifadhi historia vizuri zaidi na kuvutoa watu wengi zaidi wa ndani na nje ili kweda kujifunza historia hivyo kwa kutumia fedha hizo wataweka vifaa vya kisasa na vya kiteknolojia na hiyo itasaidia wageni wataoenda waweze kukaa muda mrefu bila kuchoka.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za mkoa wa Arusha walishiriki katika maadhisho hayo ya miaka 55 ya Azimio la Arusha walisema kuwa makumbusho hayo ni sehemu ya wao kujifunza kwa vitendo na sio kubaki kusikia tuu na kupitia maadhimio yaliyowekwa na waasisi wanaamini wakiyafuata nchi itaendelea kuwa na usalama na amani kwani kila mmoja atajua wajibu wake ni upi katika kulipeleka taifa mbele.