Home BUSINESS WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI NYAKAFURU WAIOMBA SERIKALI KUWAPATIA LESENI YA UCHIMBAJI

WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI NYAKAFURU WAIOMBA SERIKALI KUWAPATIA LESENI YA UCHIMBAJI

Na: Costantine James, Geita.

Wachimbaji wadogo wa madini   Zaidi ya elfu tatu (3000) katika mgodi wa nyakafuru uliopo wilayani mbogwe mkoani geita wameiomba serikali kuwapatia leseni ya uchimbaji wa madini katika mgodi wa nyakafuru hali inayosababisha wachimbaji wakubwa kushindwa kuwekeza katika mgodi huo.

 Walisema hayo  mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemery Senyamule wakati wa ziara ya kimadini wilayani Mbogwe (Mkoa wa kimadini)  nakusema kuwa wanaiomba serikali iwapatie leseni ya uchimbaji hali itakayowafanya wachimbaji  kuongeza uwekezaji katika machimbo hayo hivyo itawafanya wananchi wanaofanya shughuli za uchimbaji wa madini katika mgodi huo kujiongezea kipato huku  serikali itaweza kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato katika mgodi huo.

“Mhe mkuu wa mkoa changamoto kubwa tuliyo nayo katika mgodi wet wa isanjabadugu nyakafuru ni kukosa leseni ya uchimbaji madini hivyo kupelekea wachimbaji wakubwa washindwe kuja kuwekeza tunaiomba serikali yetu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inayoongozwa na jemedali wetu mama yetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya madini na ofisi yako ya mkuu wa mkoa itupatie leseni nah ii itafanya mapato ya serikali kuongezeka” alisema Patrick Emmanuel Katibu wa mgodi wa isanjabadugu .

Mkuu wa mkoa mhe. Rosemary Senyamule  wakati akijibu juu ya swala la wachimbaji la kuomba kupewa leseni ya uchimbaji mhe. Mkuu wa Mkoa amewasihi wachimbaji hao kuwa na subira wakati wizara inalishughulikia kwani wapo kwenye taratibu za mwisho kupata ufumbuzi wa suala hilo ikiwa ni baada ya Waziri mwenye  dhamana ya ya madini alipofika kwenye mgodi huo na kuwaahidii kuwapatia leseni hiyo.

“Mhe. Waziri amewahakikishia kuwa jambo hili lipo kwenye mchakato tunayoimani kubwa kuwa hata mhe. Rais anayo anatamanio ya wananchi wake kupata maeneo ya uchimbaji wale ambao hawana uwezo wa kukata leseni  mmoja mmoja  kama nyie ili muweze kupata kwa leo hatuwezi kutoa jibu la halika lakini jibu la hakika ni kuwa jambo hili bado linaendelea kwenye utaratibu lakini hatua nzuri zimefikiwa tuendelee kusubili na itakapo kamilika tutakuja kuwapa majawabu mazuri” Alisema Rosemary Senyamule Mkuu wa mkoa wa Geita.

 Mhe Senyamule alito wito kwa wachimbaji wadogo kwenye mgodi wa Nyakafuru  kuaachana na utoroshaji wa madini kwenda kuuza madini yao njee ya masoko yasiyo rasini kwani kuuza madini kwenye masoko yasiyo rasmi ni kinume na sheria huku akisema kufanya hivyo ni chanzo cha upotevu wa mapato ya serikali kwenye eneo husika. 

Vile vile amemtaka meneja wa TARURA wilaya ya Mbogwe kuhuisha mtandao wa barabara ndani ya siku 14 ili barabara ya kuelekea Mgodi wa Nyakafuru iweze kuingizwa  kwenye mtandano wa barabara za wilaya ili ijengwe na wakati huohuo amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Mbogwe kufanya marekebisho ya barabara ya kuingilia kwenye mgodi wa Nyakafuru ili iweze kupitika kwa kipindi ambacho TARURA inafanya maboresho ya mtandao wa barabara.

Meneja wa Madini Mkoa wa kimadini Mbogwe  Mhandisi Joseph Kumbulu amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Geita kuwa ofisi yake inawasimamia kikamilifu wachimbaji wa madini  pamoja na wafanyabiashara wa madini kwa lengo la kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu zilizowekwa na nchi ili kuongeza wigo wa seriksli katika ukusanyaji wa mapato huku akisema mpaka sasa zaidi ya milioni 600 imepatikana kupitia ushuru kwenye mgodi wa Nyakafuru.

“Tangu mwezi wa kumi  viongozi wameingia wamekusanya zaidi ya milioni 600 kwenye eneo hili apa kwahiyo unavyoona ule mchango wa bilioni moja kutoa kwenye lashi nusu imetoka kwenye mgodi huu hapa vile vile mgodi huu tulikuwa na changamoto ulikua haujafanyiwa usimamizi mzuri kwenye maswala ya wakaguzi tulitoa maelekezo wafanye mabadiliko kwenye timu ya ukaguzi yote waliivunja na wakaunda upya” Alisema Mhandisi Joseph Kumbulu Meneja wa Madini Mkoa wa kimadini Mbogwe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here