Home SPORTS SIMBA YAIADHIBU PRISONS 1-0 KWA MKAPA

SIMBA YAIADHIBU PRISONS 1-0 KWA MKAPA

 

Na: Stella Kessy, DAR.

KIKOSI cha Simba leo kimeibuka na ushindi katika mchezo wa ligi baada ya kuichapa Tanzania Prisons kwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Katika dakika za 78  mshambuliaji, Meddie Kagere  aliipiga penati ambayo limetosha kuipa Simba  ushindi.

Kwa ushindi huo, mabingwa watetezi wanafikisha pointi 28 katika mchezo wa 14, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi saba na vinara, Yanga SC ambao pia wana mchezo mmoja mkononi.

Tanzania Prisons hali inazidi kuwa mbaya baada ya kichapo cha leo, wakibaki na pointi zao 11 baada ya mechi 14 na kuendelea kuzibeba timu nyingine zote 15 kwenye ligi hiyo.

Katika mchezo uliotangulia, wenyeji, Ruvu Shooting walilazimishwa sare ya 1-1 na Mbeya Kwanza Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Saadat Mohamed alianza kuifungia Ruvu Shooting dakika ya 36, kabla ya Habib Kyombo kuisawazishia Mbeya Kwanza dakika ya 51.

Kwa matokeo hayo, Ruvu Shooting inafikisha pointi 12 na kusogea nafasi ya 14 na Mbeya Kwanza wanatimiza pointi 13, ingawa wanabaki nafasi ya 12 baada ya tlmu zote kucheza mechi 14.

Previous articleWAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA DUNIA NCHINI
Next articleORODHA YA LIGI BORA AFRIKA, TANZANIA YA 10
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here