Home LOCAL SIKU YA PILI UWEKAJI ANWANI YA MAKAZI JIJI LA ARUSHA JAMII...

SIKU YA PILI UWEKAJI ANWANI YA MAKAZI JIJI LA ARUSHA JAMII YAANZA KUELEWA UMUHIMU WA ZOEZI HILO

Mwenyekiti wa mtaa wa Old polisi line kata ya Themi Paulina Charles akiongea na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya zoezi la uwekaji anwani za makazi.

Mkazi wa eneo la Old polisi line kata ya Themi Witness Copriano umuhimu wa zoezi hilo kwa jamii.

Muonekano makazi yatavyokuwa na namba baada ya kukamilika kwa zoezi la uwekaji za makazi, picha hii ni mojawapo ya nyumba zilizofanyanyiwa zoezi hilo hilo kwa majaribio awali.

NA:  NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza kwa zoezi la uwekaji anwani ya makazi katika kata ya Themi jamii yaanza kuona umuhimu wa zoezi hilo kwa  kutoa  ushirikiano kwa watendakazi wanaotekeleza zoezi hilo.

Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa mtaa wa Old polisi line Paulina Charles alisema kuwa kwa siku hii ya pili Zoezi limeenda vizuri kwani wananchi wametoa ushirikiano wa kutosha tofauti na awali ambapo wengi walikuwa hawajui kama Kuna zoezi kama hilo.

“Baada ya kupitia kwenye nyumba kadhaa jana habari zimesambaa na wengi walikuwa wametarajia kufikia muda wowote lakini pia gari la matangazo limesaidia kwani hata ambaye hakuweza kupata habari kutoka kwa vyombo vya habari, ndugu, majirani amepata kupitia gari la matangazo nafikiri ndio mana Zoezi leo limekuwa rahisi tofauti na Jana,” Alisema  Bi Paulina.

Alifafanua kuwa katika mtaa wake nyumba zote zimeshafikiwa lakini bado chache ambazo wenyewe hawakuwepo na anaamini kesho watakuta wameacha taarifa zao na kuweza kukamilisha zoezi hilo katika mtaa wake.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Corridor area iliyopo ndani ya kata  Chambi Agrey alisema kuwa uelewa wa wananchi umeongezeka na zoezi linaenda kama lilivyopangwa na anatarajia wataweza kukamilisha ndani ya muda uliyowekwa.

Mmoja wa wananchi Witness Copriano  wa mtaa wa Old polisi line alisema kuwa mwanzo walikuwa hawaelewi lakini baada ya kupata elimu wameelewa kuwa zoezi hilo litarahisisha maisha kwani chochote ambacho mtu atakitaka anaweza kuagiza kwa watoa huduma na kikamfikia bila usumbufu wowote.

“Mimi naonao zoezi ni lizuri kwasababu wanavyokuja na kubanfika anwani hizo na nyumba ikaingiza katika mfumo  hata ukitaka kumfikia mtu mwingine ukishajia namba ya nyuma na mtaa anaoishi inakuwa rahisi lakini pia inatatua changamoto nyingi ikiwemo masuala ya ulinzi na usalama,”Alisema Witness.

Previous articleRAIS SAMIA AKUTANA NA TUNDU LISSU UBELGIJI
Next articleSIMBA YAICHAPA RUVU SHOOTING 7-0
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here