Home LOCAL SHIRIKA LA INADES FORMATION TANZANIA (IFTz) LATOA MICHE YA MATUNDA KATIKA SHULE...

SHIRIKA LA INADES FORMATION TANZANIA (IFTz) LATOA MICHE YA MATUNDA KATIKA SHULE MKOANI SINGIDA

Mratibu wa Mradi wa Ustawi wa Mnyama Punda wa Shirika la  Inades Formation Tanzania (IFTz)  Fortunata Tarimo akimkabidhi mche wa matunda mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ghata ya Kata ya Maghojoa kwa ajili ya kuipanda shuleni hapo katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Singida.
Mazungumzo yakifanyika kabla ya kupokelewa kwa miche hiyo.
Wanafunzi wakiwa wamebeba miche hiyo ya matunda.
Afisa Ugani wa Kata ya Msange, Benny Andrew akielekeza jambo wakati wa kupokea miche hiyo.
Wanafunzi wakibeba miche hiyo.
Miche ikibebwa.
Makabidhiano ya miche hiyo ya matunda yakifanyika.
Mwanafunzi wa Darasa la Saba Shule ya Msingi Hendeshi, Derotia Alphonce akishukuru kwa niaba ya wenzake kwa kupelekewa miche hiyo na shirika hilo.
Mwalimu Suzan  Deus wa Shule ya Msingi Hendeshi akizungumza kwenye hafla ya kupokea miche hiyo.
Miche ikichukuliwa na wanafunzi tayari kwa kupandwa.
Mwalimu  Elibariki Allan akizungumza wakati wa kupokea miche hiyo.
Baadhi ya miche iliyotolewa katika shule hizo. 

Na Dotto Mwaibale, Singida

SHIRIKA la Inades Formation Tanzania (IFTz) linalojishughulisha na Ustawi wa Mnyama Punda lenye makao makuu yake jijini Dodoma limetoa miche ya miti ya matunda 140 kwa shule za msingi wilayani Singida ili kuhifadhi mazingira na kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa zoezi la utoaji  wa miche hiyo katika Shule ya Msingi ya Hendeshi iliyopo Kata ya Msange na Ghata iliyopo Kata ya Maghojoa wilayani humo kwa uratibu wa shirika hilo, Mratibu wa Mradi wa Ustawi wa Mnyama Punda, Fortunata Tarimo alisema shabaha yao pamoja na kupigania haki za mnyama huyo pia ni kutunza mazingira.

Alisema kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo kila mtu yanamgusa wakiwamo wanyama na punda akiwepo na kukosekana kwa malisho na kusababisha punda kupelekwa mbali kutafuta malisho wakaona waanze kukabiliana na hali hiyo kwa kupanda miti si ya kivuli pekee bali na ya matunda ili na wanafunzi nao wapate lishe.

“Katika maeneo haya ipo miti kwa ajili ya kivuli lakini sisi tumeenda mbali zaidi kwa kutoa miche hiyo ya matunda kwa ajili ya kupandwa ili wanafunzi waweze kupata lishe kwani baadhi yao wanatoka mbali ya shule hivyo itakuwa ni fursa kwao kupata chakula wakati wa mchana” alisema Tarimo.

Alisema mabaki yatakayokuwa yakibaki baada ya kuliwa matunda hayo yatatumika kama chakula cha mnyama punda.

Tarimo alisema katika kila shule wamepanda miche ya matunda 70 na kuwa aina ya miche hiyo ni mahembe, parachichi, pasheni, michungwa, limau na mapera.

Aidha Tarimo  akizungumzia lengo la mradi huo alisema ni kuboresha maisha ya watu waishio vijijini kupitia mnyama punda na kuongeza uelewa wa watu juu ya haki za wanyama na ufugaji bora wa Punda,mwisho wa siku watu wanatakiwa kujua punda anatakiwa kula nini,analala wapi na anahaki gani za msingi kutoka kwa binadamu.

Aidha ameeleza mafanikio waliyopata kutokana na mradi huo ikiwa ni pamoja na kubadili mitizamo ya wananchi na kupunguzwa ukatili dhidi ya mnyama punda.

“Mafanikio yapo toka tumeanza mradi huu,maana wananchi wengi waliopo vijijini wameanza kubadilika kimtazamo juu ya mnyama punda ndio maana sasa wameanza kuacha kuuza punda” alisema Tarimo.

Afisa Ugani wa Kata ya Msange Benny Andrew alisema mpango wa kupanda miche ya matunda ulioanzishwa na shirika hilo kwa kushirikiana na Shirika la Group Tanzania utasaidia kukabiliana na uhalibifu wa mazingira unaotokana na tabia nchi hasa katika maeneo ya milima yenye mmomonyoko na kuwa matunda yatakayopatikana yatatumika kuongeza lishe kwa wanafunzi wa shule husika.

Alisema akiwa kama msimamizi mkuu wa masuala ya kilimo katika kata hiyo atausimamia mradi huo kwa karibu na kuwa endelevu na matunda yote yatakayo patikana atahakikisha yanawafikia walengwa. 

Mwanafunzi Derotia Alphonce wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Hendeshi akishukuru kwa niaba ya wenzake alilishukuru shirika hilo kwa kuwapelekea miche hiyo kupitia mradi huo ambao utawasaidia kuwapatia lishe bora kupitia matunda hayo.

Mwalimu Suzan Deus alilishukuru shirika hilo kwa mpango huo na kuahidi kuitunza miche hiyo kupitia klabu ya wanafunzi ijulikanayo kwa jina la Championi ambayo ni mlezi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here