Home LOCAL DITOPILE : RAIS SAMIA ANAZIDI KUWAFUNGA MIDOMO WALIOMBEZA UENDELEZAJI WA MIRADI DODOMA

DITOPILE : RAIS SAMIA ANAZIDI KUWAFUNGA MIDOMO WALIOMBEZA UENDELEZAJI WA MIRADI DODOMA

DODOMA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile amesema Rais Samia ndani ya muda mfupi madarakani anazidi kuwaumbua wale wote waliombeza kuhusu uendelezaji wa miradi ya kimkakati Jiji la Dodoma iliyo asisiwa na Mtangulizi wake Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. 

Mbunge Ditopile ameyasema hayo leo baada ya Hafla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuweka  Jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje katika mji wa Dodoma, Barabara hiyo itatoka Ihumwa-Matumbulu-Nala-Veyula-Ihumwa Kilometa 112.3. Hafla hiyo imefanyika kwenye Sherehe zilizofanyika leo tarehe 09 Februari, 2022 katika eneo la Veyula Jijini Dodoma

“Nampongeza kidhati Rais Samia kwa kuendelea kutimiza ahadi zake kwa vitendo za kuendeleza miradi yote ya kimkakati iliyoasisiwa na Hayati Dkt. John Magufuli Jijini Dodoma, wote ni mashahidi miradi inaendelezwa kwa kasi kubwa sana”

“Yalikuwepo Maneno kwamba Hayati ameondoka na miradi itasimama au haitafanyika lakini sasa ni tofauti, miradi yote inaendelezwa. Mradi huu wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma ni mradi ulisubiriwa kwa Hamu na wana Dodoma utalibadilisha hili jiji letu”

“mradi mwingine unaendelezwa na Rais Samia Jijini Dodoma ni ujenzi wa Hospitali Mpya ya Jiji la Dodoma na tayari Rais Samia ametoa zaidi ya Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wake kuanza, sisi wana Dodoma tunamshukuru na kumpongeza Sana”

“Rais Samia anaonyesha kwa Vitendo anayo nia ya dhati ya kuendeleza miradi yote ya mtangulizi wake, nawasihi watanzania tupuuze maneno ya watu wachache wasioitakia mema Nchi yetu, Rais Samia atatekeleza miradi yote aliachiwa tena kwa kasi kubwa na ufanisi”

“Hii Miradi Mfano Njia mchepuo Kusini Jiji la Arusha 42.4KM

– Barabara ya Mbinga-Mbamba Bay 66KM

-Barabara ya Singida, Babati, Minjingu 223.5KM

– Barabara ya Arusha-Namanga 105KM

– Iringa- Dodoma 260KM

– Namtumbo-Tunduru 190KM

– Mayamaya-Bonga 188KM

– Tunduru – Mangaka Mtambaswala 202.5KM yote inaendelea kutekelezwa na itakamilika kwa wakati, huyu ndo Rais Samia wa Vitendo sio Maneno”

Previous articleCCM SINGIDA YAZINDUA RASMI KADI ZA KIELEKTRONIKI
Next articleSHIRIKA LA INADES FORMATION TANZANIA (IFTz) LATOA MICHE YA MATUNDA KATIKA SHULE MKOANI SINGIDA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here