Home LOCAL MWANAFUNZI DARASA LA NNE AJINYONGA, HUKU MZEE MIAKA 89, AKISHIKILIWA KWA TUHUMA...

MWANAFUNZI DARASA LA NNE AJINYONGA, HUKU MZEE MIAKA 89, AKISHIKILIWA KWA TUHUMA ZA UBAKAJI.

Na: Costantine James, Geita.

Mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi  Shinamwenda alietambulika kwa jina la Saada Ndegea mwenye umri wa miaka 14 mkazi wa kijiji cha Bunegezi kata ya Ihamilo wilaya ya Geita mkoani Geita  amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya Mti.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita Kamishina msaidizi Henry Mwaibambe amesema  tukio hilo  limetokea katika kijiji cha Bunegezi kata ya Ihamilo wilaya ya Geita mkoani Geita  ambapo mwanafunzi huyo alietambulika kwa jina la Saada Ndegea mwenye umri wa miaka 14 alikutwa amejinyonga  kwenye mti wa mtundu huku chanzo cha tukio hilo ikiwa ni mwanafunzi huup kulazimishwa kwenda shule kwa miguu  katika kijiji cha Shinamwenda baada ya baiskeli aliyokuwa anaitumia kuhalibika.

“Huko maeneo ya kiji cha Bunegezi kata ya Ihamilo wilaya na Mkoa wa Geita  Saada Ndegea miaka 14 msumbwa, mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi shinamwenda alikutwa amefariki dunia kwa akujinyongakwa kamba ya mti kwenye mti wa mtundu chanzo cha kifo ni kwamba  marehemu alikua analazimishwa kwenda  kiji cha shinamwenda kusoma shule kwa miguu baada ya baiskeli yake kuharibika ndipo alipokasilika na kwenda kujinyonga.”  Alisema Henry Mwaibambe kamanda wa jeshi la poloisi mkoa wa Geita.

Katika tukio jingine Mzee  wa miaka 89, alietambulika kwa jina la Gervas Katemi mkazi wa Nyanisebeyi, Biharamulo anatuhumiwa kwa kuwabaka wajuu zake waliotambulika kwa majina ya Grace Tano miaka 20, Elizabeth Tano huku akiwatishia kutokutoa taarifa huzo kwa mtu yoyote na endapo watafanya hivyo watakufa.

“Mzee anaeitwa  Modesta Katemi miaka 54, msukuma mkazi wa Magogo alipigiwa simu na baba yake mzazi Gervas Katemi Msukuma miaka 89, mpagani mkulima mkazi wa Nyamisebeyi Biharamulo akimtaka amutumie wajujuu zake wakamsaidie kazi za kwenye mghawa huko biharamulo ndipo wajukuu wawili Grace Tano miaka 20, na Elizabeth Tano waliruhusiwa na kuweza kufika siku hiyo  hadi nyumbani kwa babu yao huko biharamulo na ilipofika majira ya saa 02:00 usiku Babu huyo alimfuata mjukuu mmoja wao ambaye ni Grace Tano amahali alipokuwa amelala na kuweza kumwingilia kimwili  yaani kubaka.” Alisema Henry Mwaibambe kamanda wa jeshi la polosi mkoa wa Geita.

Katika kikao cha kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita na viongozi wa kamati ya amani kilichofanyika leo 17.2.2022 kamanda Mwaibambe amesema katika kipindi cha miezi 6 kuanzia Agosti 2021 hadi januari 2020  mauaji ya  jumla ni watu takilibani 46 ambayo yametokea katika mkoa wa Geita huku akisema mauaji hayo yalichangiwa na ,ushirikina (2) , wivu wa mapenzi (10), mauaji ya kawaida (8), mauaji ya kihalifu (3), ugomvi wa kawaida (23).

Nao baadhi wajumbe walioshiriki katika kikao hicho wakiwemo viongozi wa dini wa madhehebu mbali mbali wamekea mauaji hayo huku wakiwataka wananchi kuwa na hofu ya mungu na kuachana na matukio yanayopeleka mpka kufikia mtu kujitia uhai wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here