Home LOCAL SERIKALI YAOMBWA KUONGEZA KASI ZOEZI LA UWEKAJI ANWANI ZA MAKAZI

SERIKALI YAOMBWA KUONGEZA KASI ZOEZI LA UWEKAJI ANWANI ZA MAKAZI

Wataalamu wa utambuzi wa uwekaji anwani za makazi wakiweka namba katika nyumba mbalimbali zilizopo katika mtaa wa Themi Mashariki kata Themi.

Mwenyekiti wa mtaa wa Themi Mashariki kata ya Themi Godfrey Mushi akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na zoezi la uwekaji anwani za makazi.

Mkazi wa mtaa wa Themi Mashariki kata ya Themi Godfrey Mgwasa akiongea na waandishi wa habari.

Magreth Ignatus mkazi wa mtaa wa Themi Mashariki kata Themi jiji la Arusha akiongea na waandishi wa habari.

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA 

Ikiwa Leo ni siku ya mwisho zoezi la utambuzi wa anwani za makazi unaoendelea katika tano za jiji la Arusha ili kuingia kwenye hatua nyingine  ya uwekaji wa majira ya nukta(Code Net)  Wananchi wa kata ya Themi mtaa wa Themi Mashariki wameiomba serika kuongeza kasi  ili waweze kunufaika na mfumo huo utakarahisisha mambo mengi ikiwemo biashara zao.

Godfrey Mgwasa mkazi wa mtaa huo alisema kuwa kama walivyosikia malengo ya zoezi hilo ni kwa manufaa ya wananchi na nchi kwa ujumla ni vema ikafanyika kwa wakati na haraka inayotakiwa  na kumaliza mapema ili matumizi ya mfumo huo yaanze ili kuwanufaisha wananchi.

“Serikali waongeze spidi kwani tumechelewa ukilinganisha na nchi nyingine zilizoendelea tunatamani matumizi ya mfumo huu ionekane mapema,” Alisema Mgwasa.

Magreth Ignatus ambaye pia ni mkazi wa kata hiyo alisema  ameelewa kuwa zoezi hilo lina faida kubwa kwani baada ya kukamili wakiwa majumbani anaweza kuagiza bidhaa na zikamfikia bila shida yoyote.

“Kama Mimi kulingana na hii biashara yangu ya duka na mboga mboga na matunda naamini nitaweza kuagiza machingwa nyanya na bidhaa zingine na hii itanirahisishia mimi kuokoa muda lakini pia kufanya shughuli zingine za nyumbani wakati nasubiri mzigo niliouagiza ufike,” Alisema Bi Magreth.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Themi Mashariki kata ya Themi   Godfrey Mushi alisema kuwa tangu kuanza kwa zoezi hilo la utambuzi wa uwekaji anwani za makazi zoezi limeenda vizuri lakini pia zinapotokea changamoto ndogo ndogo wanazirekebisha na zoezi linaendelea kufikia lengo.

“Leo tunaenda vizuri zaidi kuliko jana  na juzi kwasababu watu wengi wameelewa juu zoezi hili na wale ambao tunakuta hawapo tunazipa nyumba namba na kuwaachia majirani fomu kwaajili ya kutoa taarifa zao na baadae tutakuja kuzipitia,” Alisema Mushi.

Hata hivyo manufaa ya mfumo huo ni kurahisisha utoaji, upatikanaji na upelekaji wa huduma kwa wananchi au wateja, Kuongeza wa ukusanyaji mapato, kuongeza ajira, kuimarisha ulinzi na usalama, kurahisisha upatikanaji wa huduma majumbani pamoja na Kuimarisha biashara kwa njia ya mtandao.

Previous articleWIZARA YA AFYA YAPOKEA VIFAA VYA TEHAMA VYENYE THAMANI ZAIDI YA MIL. 105
Next articleMWANAFUNZI DARASA LA NNE AJINYONGA, HUKU MZEE MIAKA 89, AKISHIKILIWA KWA TUHUMA ZA UBAKAJI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here