Home LOCAL MHE. MARY MASANJA AWATAKA WANANCHI KUACHA KUMEGA MAENEO YA HIFADHI

MHE. MARY MASANJA AWATAKA WANANCHI KUACHA KUMEGA MAENEO YA HIFADHI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka wananchi kuacha kuomba kumegewa maeneo ya Hifadhi ili kuepukana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu.

Amesema hayo leo Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipompa nafasi ya kujibu kuhusu changamoto ya wanyama wakali na waharibifu mkoani humo.

Amesema kuwa ili kukabiliana na changamoto hiyo, vikosi kazi vitatumwa katika maeneo yenye changamoto ya wanyama wakali na waharibifu.

Aidha,ameahidi kutekeleza maelekezo ya Rais ya kuhakikisha Wizara inaweka Kambi ya kudumu kwenye maeneo yenye changamoto ya wanyama wakali na waharibifu.