Home BUSINESS KUWEPO KWA TAARIFA ZA UONGO KUHUSU AJIRA BENKI KUU

KUWEPO KWA TAARIFA ZA UONGO KUHUSU AJIRA BENKI KUU

Kuna barua pepe feki inayosambaa mitandaoni kuhusu kuwepo kwa mchakato wa ajira Benki Kuu wa kuchukua wafanyakazi kutoka Taasisi mbali mbali za Fedha. Taarifa hizi hazina ukweli wowote, hivyo zipuuzwe.

Barua pepe hiyo feki ya tarehe 5 Februari, 2022 yenye kichwa cha habari “OMBI LA KUKUAJIRI BOT” ambayo inaonesha kutumwa kupitia barua pepe ya Benki Kuu ya info@bot.go.tz imemtaka aliyeandikiwa kuwasilisha maombi yake ya ajira kupitia barua pepe ya esamson048@gmail.com.

Aidha, taarifa hiyo feki inaonesha kuwepo kwa mawasiliano kati ya mtu aitwaye Irene Millinga (millingairene42@gmail.com) na mtu aitwaye Dr. Tefilo Richard (tefilor1@gmail.com ) tarehe 8 na 9 Februari, 2022 kupitia barua pepe yenye kichwa cha habari  “MCHAKATO WA AJIRA BOT”.

Taarifa hizi zote ni za uongo. Bila shaka zimeandaliwa na watu wenye nia ovu ili kuwatapeli watu kwa imani kuwa watapata ajira Benki Kuu. Hakuna mchakato wowote wa ajira unaoendelea Benki Kuu kwa kuchukua wafanyakazi kutoka Taasisi mbali mbali za Fedha.

Hivyo, taarifa hizo zipuuzwe. Aidha, tunawaonya watu wanaojihusisha na kutunga taarifa za uongo za namna hii kuacha mara moja kuepuka hatua za kisheria dhidi yao. 

Imetolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki botcommunications@bot.go.tz

Previous articleSERIKALI KUGHARAMIA MATIBABU YA PROF. JAY MUHIMBILI
Next articleWIZARA YA AFYA YAPONGEZA WADAU NA WAFADHILI WA MAENDELEO, WANAOFADHILI MRADI WA MAFUNZO KWA VITENDO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here