Home SPORTS KOCHA PABLO AJIPANGA KIVINGINE

KOCHA PABLO AJIPANGA KIVINGINE

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Na: Stella Kessy

KOCHA mkuu wa klabu ya Simba Pablo Franco amesema kuwa ataingia kivingine kutokana na hali ya kikosi kilivyo.

Pablo amesema baada ya mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika  dhidi ASEC Mimosas kuna baadhi ya wachezaji walipata maumivu hivyo hawakuwa sehemu ya mechi ya leo

Pablo ameongeza kuwa anategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Ruvu na mchezo utakuwa mgumu lakini licha ya kukosa muda wa maandalizi tunahitaji kushinda ili tufuzu hatua inayofuata.

“Kutakuwa na mabadiliko kidogo ya kikosi na tutaingia kivingine, baada ya mechi ya juzi hatujapata muda wa kuweka miili sawa lakini tunahitaji kushinda” amesema

“Tulikuwa katika kiwango bora kwenye mchezo uliopita, tunakwenda kukutana na timu bora na hii ni mechi ya mtoano kwahiyo tunapaswa kuhakikisha tunakuwa makini ni muhimu kwetu kuingia hatua inayofuata” amesema