Home SPORTS KMC YAILIPUA POLISI TANZANIA 3-0

KMC YAILIPUA POLISI TANZANIA 3-0

Na: Stella Kessy DAR.

KIKOSI cha KMC leo imelipa kisasi mbele ya Polisi Tanzania kwa kuwatungua mabao 3-0 na kusepa na pointi tatu mchezo  uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Huku katika mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Karatu,  Polisi Tanzania 2-0 KMC na kuwafanya waweze kusepa na alama 3.

Mabao yalijazwa kimiani na Idd Kipagwile dk 15, Emmanuel Mvuyekule dk 73 na Sadalla Lipangile dk 88.

Ushindi huo unaifanya KMC kufikisha pointi 22 ikiwa nafasi ya 6 na Polisi Tanzania inabaki na pointi 19 ikiwa nafasi ya 9 katika msimamo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here