Home SPORTS KIDUKU KUZICHAPA MWEZI UJAO

KIDUKU KUZICHAPA MWEZI UJAO


Na: Stella Kessy, DAR.

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Twaha Kiduku amesaini mkataba wa kupanda ulingoni kuzichapa dhidi ya Alex Kabangu kutoka DR Congo katika pambano litakalopigwa Machi  26, mwaka huu  Mkoani Morogoro.

Kiduku atapanda ulingoni kwenye pambano hilo la Kimataifa dhidi ya Kabangu baada ya kumchakaza Dullah Mbabe mwezi Agosti mwaka jana kwenye pambano la Usiku wa Deni lililopigwa Ubungo Plaza, Dar es salaam

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Kiduku amesema sapoti anayopewa na watanzania inazidi kumpa uwezo wa kufanya vizuri katika kila pambano huku akiahidi kuiandika historia kwa Mara nyingine kwa kumchakaza Vibaya Alex Kabangu.

“Ni kweli nimesaini kucheza pambano hilo ambalo litakuwa la mkanda wa ubingwa, naamini mkanda utabakia kwa sababu lazima nifanye maandalizi ya kutosha chini ya kocha wangu Pawa Ilanda na nguvu kubwa ninayo pewa na mashabiki zangu kwanza wa Morogoro na Watanzania Wote kwa Ujumla ambao hawajawahi kuniacha Tangu siku ya kwanza”

“Kila kitu tayari kimeshapangwa na promota juu ya siku ya pambano lakini maombi yangu ni kuweza kuwezasha pambano kufanyika mjini ili watu wengi waweze kuhudhuria taofauti na Magadu kwa sababu ni mbali na mjini.

Aidha Mratibu Mkuu kutoka Peaktime Media Meja Selemani Semunyu amesema pambano hilo la kimataifa litasindikizwa na Mabondia Nyota wa Morogoro akiwemo Joseph Mchapeni Dhidi ya Ally Mwerangi,  Juma misari dhidi ya kareem Mandonga,  Ayubu Mwankina na Wengine Wengi.

Mwisho.

Previous articleWATUMISHI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAHIMIZWA KUUTANGAZA UTALII WA NDANI NA NJE NCHI
Next articleMORRISON AREJESHWA KIKOSINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here