Home SPORTS GEITA GOLD FC YABANWA MBAVU NA NAMUNGO FC DIMBA LA NYANKUMBU...

GEITA GOLD FC YABANWA MBAVU NA NAMUNGO FC DIMBA LA NYANKUMBU GEITA

Na: Costantine James, Geita.

Ligi kuu Tanzania bara NBC Premier leage imeendelea hii leo kwa mchezo mmoja uliopigwa mkoani Geita katika dimba la Nyankumbu stadium ambapo matajir wa dhahabu wa mkoa wa Geita, Geita Gold Fc waliwakalibisha timu ya Namungo FC katika kuzisaka pointi tatu mhimu ndani ya Ligi kuu Tanzania bara.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la nyankumbu Stadium majira ya saa kumi mchezo huo ulikuwa wa vuta nikuvute huku kila timu ikitaka kupata bao kwa lengo la kujihakikishia kuondoka na pointi zote tatu mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinatamatika hakuna timu yoyote iliyoweza kuliona lango la mwenzake si Geita Gold Fc ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo wala Namungo Fc.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi timu zote zikitafuta kupata gori Timu ya Geita Gold FC ikawa yakwanza kuwanyanyua mashabiki wake kupitia kwa mchezaji wake machachali hapa namzungumzia  George Mpole ambae hakuonesha upole kwa timu ya Namungo Fc dakika ya 73 George akazitikisa nyavu za Namungo nakufanya ubao wa matokeo usome moja kwa sifuri.

Lakini juhudi za Geita Gold za kuhakikisha wanabakiza pointi zote tatu katika dimba la nyankumbu hazikufua dafu mbele ya Namungo Fc baada ya Idd Farjala kusisawazishia timu hiyo kunako dakika ya 84 nakufanya ubao usome 1-1.

Mpaka dakika 90 za mwamuzi zinakamilika za mchezo huo hakuna mbame baada ya kugawana ponti moja moja huku Geita Gold hasira za kutaka kulipiza kisasi kwa timu hiyo kwani mchezo wa mzunguko wa kwanza walipoteza mbele ya Namungo fc kwa kuchapwa mabao 2-0.

Mara baada ya mchezo huo mashabiki wa Geita Gold Fc waliojitokeza kuja kuipa sapoti timu yao pamoja na viongozi wa timu wakaipongeza timu yao kwa mwenendelezo mzuri wa  matokeo licha ya kugawana alama moja na timu ya Namungo huku wakituma salamu kwa timu ya wananchi kwani mchezo ujao Geita gold watakipiga na Yanga sport club.

Baada ya mchezo huo timu zote mbili zimesalia pale pale katika msimamo wa ligi kuu Tanzanaia bara ambapo Geita Gold Fc imesalia nafasi ya 6 ikiwa imejikusanyia alama zake 21 katika michezo yake 16 huku Namungo Fc ikisalia nafasi ya 4 ikiwa imejikusanyia kibindoni alama zake 24 katika michezo 16 iliyocheza mpaka sasa.

Previous articleTILIONI 1.66 ZATOLEWA KUIMARISHA SEKTA YA AFA
Next articleUPANGA MASHARIKI WAZINDUA KAMPENI KUPAMBANA NA UVIKO 19
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here