Home LOCAL DC MTANDA: HATUTAKI KUONA MTOTO ANARUDISHWA NYUMBANI KWAKUKOSA SARE YA SHULE

DC MTANDA: HATUTAKI KUONA MTOTO ANARUDISHWA NYUMBANI KWAKUKOSA SARE YA SHULE

Mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda akiongea katika hafla ya kukabidhi sare za shule kwa wanafunzi 413 iliyofanyika jiji la Arusha.

Meneja wa benki ya NMB kanda ya Kaskazini Dismas Prosper akiongea katika hafla ya kukabidhi sare za shule ikiwemo mabegi 100 yaliyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo.
Mkurugenzi jiji la Arusha Dkt John Pima akitoa taarifa ya zoezi la kusaidia wanafunzi wenye uhitaji katika jiji hilo.


Mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda akigawa mabegi ambayo na sare za shule kwa wanafunzi wenye uhitaji jiji la Arusha.

Baadhi ya wanafunzi wenye uhitaji jiji la Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa jiji hilo katika hafla ya kukabidhi mabegi 100 na sare za shule kwa wanafunzi 413.

Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya jiji Arusha wakiwa katika hafla ya kukabidhi sare za shule kwa wanafunzi wenye uhitaji.

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

 Mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda amewaonya walimu wakuu na wakuu wa shule kufuata taratibu na maelekezo halali  yanayotolewa na viongozi wa serikali  katika suala zima la sare za shule na sio kuwarudisha wanafunzi nyumbani.

Mtanda ameyasema hayo katika hafla ya kukabidhi sare za shule kwa wanafunzi 413 na mabegi 100 yalitolewa na jiji la Arusha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya NMB ambapo alisema kuwa kumekuwa na tabia ya walimu kuwapa adhabu wanafunzi ambao hawana sare za shule ikiwemo kuwarudisha nyumbani ikiwa wao hawahusiki katika ununuzi.

“Wanahusika na masuala ya ununuzi wa sare za shule ni wazazi hivyo msiwarudishe watoto na wengine tumesikia mnawatembeza peku badala yake waiteni wazazi na kuwaelekeza kununua na kama mzazi hana uwezo ni jukumu lako mkuu wa shule kwenda kueleza jambo hili kwa mkurugenzi ili mtoto huyo asaidiwe,”Alisema Mtanda.

Sambamba na hilo pia aliwataka wakuu hao kuchangisha michango yenye tija katika kuboresha taaluma  ambayo itakuwa halali kwa kufuata utaratibu wa michango na  lazima  ipitishwe na kamati ya shule na Kisha kwenda kwa Mkurugenzi na baadaye Mkuu wa wilaya na kupitishwa na mkuu wa mkoa kisha kupitishwa ndipo ianze kuchangishwa.

“Yeyote atayechangisha bila kufuata utaratibu huo anayeonyesha dalili ya kumfarakanisha Rais na wananchi hiyo lazima achukuliwe hatua hivyo wazazi wachangishwe michango yenye tija ikiwemo wanafunzi kupata chakula shuleni ili wanafunzi waweze kufanya vizuri,”Alieleza Mtanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt John Pima alisema kuwa zoezi hilo la kusaidia wanafunzi wenye uhitaji lilianza  tarehe 17 Januari 2022 kwa kugawa vifaa vya shule vya kujifunza kwa wanafunzi 413 ambapo waliahidi pia kutoa share za shulekwa wanafunzi hao ambao wameweza kulitekeleza hilo.

“Leo tunatoa unifoam kwa maana ya sketi, shati na suruale 413 kwa wanafunzi lakini pia tabegi  100 kutoka kwa benki ya NMB na naomba wadau wengine waendelee kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu 6 Samia Hassan Suluhu hasa katika nguvu kubwa aliyoiweka katika sekta ya elimu.

Naye meneja wa benki ya NMB kanda ya Kaskazini Dismas  Prosper alisema kuwa benki hiyo kila mwaka imekuwa ikitenga asilimia 1 ya faida yake kwaajili ya kurudisha kwa jamii lakini pia wafanyakazi wamekuwa wakitoa michango yao ya hiari kutoka katika mishahara yao  angalau mara 3 kwa mwaka na kusaidia makundi mbalimbali.

“Wafanyakazi wamejichanga na kidogo  na kuweza kununua mabegi haya 100 yenye thamani ya milioni 2,240,000 na jumatatu ya wiki ijayo tutakabidhi mabegi mengine 100 ambapo itafanya jumla kuwa mabegi 200 yenye thamani ya milioni 4,440,000,”Alisema meneja huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here