Home BUSINESS MELI YA MV MBEYA II KUANZA KUFANYA KAZI HIVI KARIBUNI

MELI YA MV MBEYA II KUANZA KUFANYA KAZI HIVI KARIBUNI

  
Naibu Mkurugenzi wa Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 23, 2022 wakati akifafanua juu ya Usafiri wa meli zilizopo katika Ziwa Nyasa.

MAMLAKA ya Bandari Tanzania (TPA) imesema Meli ya MV Mbeya II itaanza kufanya kazi ya kusafirisha abiria na Mizigo hivi karibuni ikiwa ni baada ya kupata dhoruba ya Upepo na Mawimbi Mei, 2021.


Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka wakati akifafanua juu ya usafiri wa Meli katika ziwa Nyasa kwa waandishi wa habari leo Februari 23, 2022 jijini Dar es Salaam. Amesema Meli hiyo imekatiwa Bima na taratibu za kiofisi zinaendelea ili kuweza kupatikana kwa fedha za Bima kwaajili ya kununua mtambo (Main Engine) mpya kwaajili ya kuwekwa ili iweze kuanza kazi tena.

Amesema kuwa mapema Meli hiyo ilipigwa na dhoruba na ikasababisha kuharibika hivyo ikalazimu kuipandisha chelezo kwa matengenezo.

Amesema kuwa matengenezo hayo yalikamilika na Meli ikapata vibali vyote vya kuendelea na kazi ilipofika Januari 27, 2022 lakini Mapema Februari 2022 Meli hiyo ikiwa kwenye safari zake za kawaida ikapata hitilafu kwenye mtambo wake mmoja wa kuendeshea ambapo iliharibika Mkono wa Piston moja.

Mhandisi Mattaka amesema kuwa utafiti umeonesha kuwa tatizo hilo lilitokana na ‘Material Failure’ na sio mapungufu ya kiuendeshaji.

Serikali kupitia TPA inaendelea kupunguza tatizo la Usafiri wa abiria na uchukuzi kwenye ziwa Nyasa ikijenga vyombo vya usafiri majini vitatu ambapo meli ya mizigo ilijengwa kwa Shilingi Bilioni 5.5 na meli ya abiria na mizigo ilijengwa kwa shilingi Bilioni 9.

Previous articleDC MTANDA: HATUTAKI KUONA MTOTO ANARUDISHWA NYUMBANI KWAKUKOSA SARE YA SHULE
Next articleWADAU WAKIOMBA CHUO CHA TAIFA CHA UTALII KUFUNGUA TAWI LAKE MIKOA YA KUSINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here