Home SPORTS CHAMPION WA KITAA KUUNGURUMA DAR LIVE KESHO

CHAMPION WA KITAA KUUNGURUMA DAR LIVE KESHO

Na: Stella kessy, DAR

JUMLA ya mabondia 20 kesho wanashuka ulingoni katika pambano la Champion wa Kitaa watakaocheza katika hatua  ya Nusu  fainali ya michuano hiyo.

Hata hivyo leo mabondia hao wamefanikiwa  kupima uzito katika  katika Uwanja wa Mbagala Zakhem tayari kwaajili ya kumenyana kesho katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala.

Akizungumza na wanahabari mratibu  wa pambano hilo Bakari Hatibu amesema kuwa kuelekea pambano hilo maandalizi yamekamilika  kwa asilimia 80 kufikia pambano hilo huku akitaja kuwa  kiingilio ni elfu 3 kwa kila mtu.

Ameongeza kuwa kesho wanatarajia kufunga ulingo wa pambano hilo ila taratibu zote za kimechezo zimekamilika ikiwemo kupima uzito na afya pamoja na mabondia kusaini  mapambano watakayocheza .

“Nategemea kuwa na mapambano kumi(10) kesho  ambapo tulianza na mapambano 20 na sasa tumefika 10 ambapo tunaimani kesho tutapata mapambano 5 yatakayotinga  fainali ambayo baada ya hapa tutajua wapi fainali itafanyika kama ni Dar live au Chamanzi Complex “amesema.

Ameongeza kuwa lengo la kuchezesha pambano la kitaa ni kutambua thamani ya ngumi na kuonyesha umuhimu wa ngumi.

Pia mabondia  watakaopanda ulingoni kesho ni Mkongwe wa Muda mrefu Shaban Kaoneka dhidi ya Ramadhan Adam, Mrisho Mzezela atazichapa dhidi ya  Osward Maneno, huku Bakari Kitogo dhidi ya Omary Matimbwa.

Bondia  Shaban Kimimbi atazinyuka dhidi ya  Bernad Fusi, huku David Edward dhidi ya Said Uwezo,  na Enock Enock atashushuka ulingoni  na  Sebastian Deo, 

bondia Jadi Swaleh atazichapa na Hussein Mkalekwa, na Swahib Ramdhan atapanda kumkabili  Antony Peter na  Zahoro Salum akimaliza na Peter Tosh,huku Pambano kuu likiwa ni kati ya Hamadi Furahisa na Maganga Kulwa.

Ametoa wito kwa wana mbagala kujitokeza kwa wingi katika pambano hilo ambalo lina usalama wa kutosha pamoja na bei nafuu kwa watazamaji.

Previous articleDKT. CHAULA ATOA WITO KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI
Next articlePATA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO J.PILI FEBRUARI 20-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here