Na: Stella kessy, DAR
JUMLA ya mabondia 20 kesho wanashuka ulingoni katika pambano la Champion wa Kitaa watakaocheza katika hatua ya Nusu fainali ya michuano hiyo.
Hata hivyo leo mabondia hao wamefanikiwa kupima uzito katika katika Uwanja wa Mbagala Zakhem tayari kwaajili ya kumenyana kesho katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala.
Akizungumza na wanahabari mratibu wa pambano hilo Bakari Hatibu amesema kuwa kuelekea pambano hilo maandalizi yamekamilika kwa asilimia 80 kufikia pambano hilo huku akitaja kuwa kiingilio ni elfu 3 kwa kila mtu.
Ameongeza kuwa kesho wanatarajia kufunga ulingo wa pambano hilo ila taratibu zote za kimechezo zimekamilika ikiwemo kupima uzito na afya pamoja na mabondia kusaini mapambano watakayocheza .
“Nategemea kuwa na mapambano kumi(10) kesho ambapo tulianza na mapambano 20 na sasa tumefika 10 ambapo tunaimani kesho tutapata mapambano 5 yatakayotinga fainali ambayo baada ya hapa tutajua wapi fainali itafanyika kama ni Dar live au Chamanzi Complex “amesema.
Ameongeza kuwa lengo la kuchezesha pambano la kitaa ni kutambua thamani ya ngumi na kuonyesha umuhimu wa ngumi.
Pia mabondia watakaopanda ulingoni kesho ni Mkongwe wa Muda mrefu Shaban Kaoneka dhidi ya Ramadhan Adam, Mrisho Mzezela atazichapa dhidi ya Osward Maneno, huku Bakari Kitogo dhidi ya Omary Matimbwa.
Bondia Shaban Kimimbi atazinyuka dhidi ya Bernad Fusi, huku David Edward dhidi ya Said Uwezo, na Enock Enock atashushuka ulingoni na Sebastian Deo,
bondia Jadi Swaleh atazichapa na Hussein Mkalekwa, na Swahib Ramdhan atapanda kumkabili Antony Peter na Zahoro Salum akimaliza na Peter Tosh,huku Pambano kuu likiwa ni kati ya Hamadi Furahisa na Maganga Kulwa.
Ametoa wito kwa wana mbagala kujitokeza kwa wingi katika pambano hilo ambalo lina usalama wa kutosha pamoja na bei nafuu kwa watazamaji.