Home BUSINESS BoT: VIJANA WA KITANZANIA WAMEFAIDIKA NA MIFUKO YA UDHAMINI WA ELIMU YA...

BoT: VIJANA WA KITANZANIA WAMEFAIDIKA NA MIFUKO YA UDHAMINI WA ELIMU YA MWALIMU NYERERE NA GILMAN RUTIHINDA

Afisa Mkuu Rasilimali Watu, Kurugenzi ya Utumishi na Maendeleo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Kashindye Sekule Phelician akiwasilisha mada kuhusu “Maendeleo ya Mifuko ya Udhamini wa Elimu ya juu inayodhaminiwa na Benki Kuu ya Tanzania” kwenye semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha iliyoandaliwa na BoT na kufanyika jijini Mbeya.

   Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada hiyo.

Mfuko wa Udhamini wa Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere (Mwalimu Nyerere Memorial Scholarship Fund) ulianzishwa na Benki Kuu ya Tanzania BoT Octoba, 2009 kwa ajili ya kuenzi mafanikio ya Rais wa awamu ya kwanza Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na ule wa Gilman Rutihinda ulioanzishwa  mwezi Machi, 1994 kwa ajili ya kumbukumbu ya aliyekuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Gilman Rutihinda ili kusaidia watoto wa kitanzania wenye vipaji kujiendeleza kwaajili ya masomo ya elimu ya juu.

Mfuko huu ulianza kwa kuchangiwa fedha na Benki Kuu ya Tanzania na taasisi zingine za fedha, viongozi wastaafu, wafanyakazi wa Benki Kuu na wananchi wengine kupitia Harambee (Fund Raising) zilizoandaliwa kwa ajili ya kutunisha mifuko hiyo.

Akizungumza wakati Akiwasilisha mada ya “Maendeleo ya Mifuko ya Udhamini wa Elimu ya juu inayodhaminiwa na Benki Kuu ya Tanzania” kwenye semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha iliyoandaliwa na BoT na kufanyika jijini Mbeya,  Afisa Mkuu Rasilimali Watu, Kurugenzi ya Utumishi na Maendeleo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Kashindye Sekule Phelician Amesema Fedha hizo ziliwekezwa kwenye dhamana za serikali (Treasury Bill na Bond) ili Mfuko uwe endelevu na faida inayopatikana tu ndiyo inatumika kufadhili wanafunzi katika vyuo vikuu hapa nchini.

Ufadhili huu umeongeza hamasa kwa wanafunzi wa kike hapa nchini wenye ufaulu wa juu katika masomo ya Hisabati na Sayansi, ili kujiendeleza kwenye masomo ya shahada na uzamili.

Hii ni kwa sababu idadi ya Wanafunzi wa kike kwenye masomo hayo imekuwa chini kwa muda mrefu.

Amesema ilichukuliwa kuwa wanafunzi wa kike kama kundi lenye uhitaji  hivyo Ufadhili huu utasaidia kuhamasisha wanafunzi hasa wa kike kufanya vizuri kwenye masomo hayo, na hivyo kuleta usawa au uwiano wa kijinsia kitaaluma kwenye masomo haya muhimu yanayochangia maendeleo ya taifa.

Aidha amefafanua kuwa Ufadhili huo unajumuisha gharama zote za ada, pesa za kujikimu, mafunzo ya vitendo na vifaa vya kujifunzia ikiwemo kompyuta mpakato (Laptop). na unatolewa kwa wanafunzi raia wa Tanzania wenye ufaulu wa kiwango cha juu waliosajiliwa vyuo vikuu nchini vinavyotambulika na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU).

“Toka ufadhili huo uanze idadi ya wanafunzi wanaofadhiliwa na mfuko huu imeongezeka kutoka wanafunzi sita (6) kama ilivyokuwa hapo awali hadi wanafunzi kumi (10) kuanzia mwaka huu wa fedha wa 2021/2022 haya ni mafanikio ya mfuko katika ufadhili huo,” Amesema Bi. Kashindye Phelician.

Amesema BoT itaendelea kuwekeza kwenye dhamana za Serikali yaani Treasury Bonds ili kuongeza uwezo wa kifedha wa mfuko huo hivyo kuongeza idadi ya wanafunzi zaidi wanaofadhiliwa kupitia Mifuko ya Udhamini wa Elimu ya Juu ya Gilman Rutihinda na ule wa Julius Kambarage Nyerere.

CREDIT: Fullshangwe Blog

Previous articleWAISHUKURU PURA KWA KUPIGANIA USHIRIKI WA WATANZANIA
Next articleRAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AZUNGUMZA NA CHEMBA YA BIASHARA, VIWANDA NA KILIMO YA UBELGIJI, LUXEMBOURG, AFRIKA, CARIBBEAN NA PACIFIC (CBL-ACP), BRUSSELS NCHINI UBELGIJI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here