Home LOCAL ZAIDI YA WANANCHI ELFU 63 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI MGANZA-BWONGERA, CHATO

ZAIDI YA WANANCHI ELFU 63 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI MGANZA-BWONGERA, CHATO

Na: Paul Zahoro,  Geita RS.

Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Geita leo Januari 15, 2022 imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani Chato na kufurahishwa na Mradi wa maji wenye thamani ya Bilioni 5.6 ambapo utakapokamilika utanufaisha zaidi ya wananchi elfu 63 kutoka kwenye vijiji 14.

“Mradi huu ni mzuri na unategemea kuhudumia watu wengi sana, kikubwa tunataka tuone umeme unawekwa ili mradi uanze kutoa huduma kwa wananchi hawa wengi wanaosubiria” Mhe. Said Kalidushi.

“Mradi wa Maji wa Mganza- Bwongera una thamani ya Bilioni 5.6 na unahudumia vijiji 14 vilivyopo kwenye Kata tatu za Mganza, Kigongo na Bwongera na utakamilika ifikapo Aprili 30, 2022 na utanufaisha wananchi elfu 63.” Mhandisi Frank Msaki, Kaimu Meneja RUWASA, Chato.


Awali, kamati hiyo ilitembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa Madarasa kwenye shule za Sekondari Buhingo Chato na Shikizi ya msingi Mkombozi ambapo imepongeza usimamizi wa miradi hiyo na imeagiza kukamilisha kasoro ndogo zilizobainika kabla ya wanafunzi kuanza masomo.

“Tunamshukuru mwananchi mmoja aliyetuuzia eneo hili kwa gharama za chini na hatimaye tumepata shule hii shikizi ya Mkombozi ambayo kwa fedha za Uviko 19 tumepata mradi wa kujenga Madarasa haya matano.” Raphael Masambo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya. 

“Niwapongeze kwanza kwa usimamizi mzuri wa majengo lakini vifaa ambavyo vipo humu ndani haviridhishi madawati yana kiwango cha chini na mtoto atakayekaa ataumia na madirisha hayawezi kufunguka maana yake watoto watavunja vioo watapokua wanajaribu kufungua.” David Azaria, Katibu Mwenezi CCM Mkoa.

Vilevile, Kamati ya Siasa ya Mkoa imekagua Mradi wa Ujenzi wa Barabara za Ntarambe- Vijana-Leahnsabi ya kiwango cha lami zenye  KM 02 unaotekelezwa kwa Tshs. 1,007,132,000 fedha kutoka Mfuko wa Barabara na imepongeza kwa mradi utakaohudumia wananchi kwa muda mrefu na imeagiza kutunzwa kwa mradi huo


Watu wengi nchini walionufaika na biashara wameanzia kuendesha bodaboda endeleeni kushirikiana na Halmashauri na jaribuni kubuni miradi mingine zaidi.” Amesema Mwenyekiti wa CCM Mkoa akiwa kwenye kikundi cha Bodaboda cha vijana Mpogoroni waliokopeshwa milioni 35 na Halmashauri.

“Nawaombe muwe waaminifu, tufanye marejesho kupitia bodaboda hizi ili vijana wengine nao waweze kukopeshwa na kufanya miradi mbalimbali ya kujiinua kiuchumi.” Richard Jaba, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa akizungumza na kikundi cha Bodaboda Mpogoroni.

Aidha, Kamati ya Siasa imekagua ukamilishaji wa hospitali ya kanda ya Chato yenye eneo la ekari 248 ambayo uenzi wake una awamu mbili ambapo ya kwanza imefikia 98% na mengine kama jengo la mionzi limefikia 90%  ikitarajiwa kudumia zaidi ya wagonjwa 1000 wa huduma za nje na 800 watakaolazwa.

“Huduma za hapa ni za kisasa na ndio zile tulikua tunazipata India miaka ya nyuma, endeleeni na moyo huo kwa kuwahudumia wananchi vizuri kwani inatupa heshma kama Chato, Geita na Taifa kwa ujumla”, amesema Mhe. Kalidushi.

Previous articleMAJALIWA: UJENZI WA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM NI SAHIHI WAZIRI
Next articleSERENGETI YABORESHA MAENEO YA UTALII, WAONGEZA VIBAO MAALUMU VYA MAELEZO YA VIVUTIO ENEO LA MORU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here