Home BUSINESS SERENGETI YABORESHA MAENEO YA UTALII, WAONGEZA VIBAO MAALUMU VYA MAELEZO YA VIVUTIO...

SERENGETI YABORESHA MAENEO YA UTALII, WAONGEZA VIBAO MAALUMU VYA MAELEZO YA VIVUTIO ENEO LA MORU
NA: MWANDISHI WETU.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kupitia Hifadhi yake ya Serengeti limeboresha shughuli za Utalii na kuongeza uzoefu kwa watalii wanaotembelea kwa kujenga vibao maalumu (interpretative panels) vyenye maelezo katika sehemu hizo za vivutio.

Kwa mujibu wa Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi na Mawasiliano kutoka TANAPA, SAC CC. Pascal Shelutete amesema kuwa, vibao hivyo maalum vitakuwa ni chachu kwa wageni wanaotembelea hifadhini kujionea vivutio vya kiutamaduni vilivyopo ndani ya eneo la Moru katika Hifadhi hiyo ya Serengeti.

“Sambamba na Watalii kupata fursa ya aina yake ya kuona Faru weusi ndani ya eneo la Moru pekee, watalii  watapata maelezo ya vivuvito vya kitamaduni kupitia vibao hivyo hivyo.

Kwani uboreshaji huu ni wa kipekee kupitia vibao hivyo vilivyojengwa kwa ubora mkubwa vikiwa na maelezo ya maisha ya kabila la Dorobo na Masai namna walivyoishi na wanyamapori, matambiko yao na wanyama walioheshimika zaidi na kwanini.” Alisema SAC CC Pascal Shelutete.

Na kuongeza: “Karibu Serengeti kwa uzoefu wa kipekee ndani ya eneo la Moru ambapo utafurahia kuona faru weusi  na historia na tamaduni za watu wa kale  kama ‘Masai rock paints’,  ‘Gong rocks’  na Historia ya wanyama adimu aina ya Faru weusi.” Alimalizia SAC CC Pascal Shelutete. 

Mwisho.

Previous articleZAIDI YA WANANCHI ELFU 63 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI MGANZA-BWONGERA, CHATO
Next articleRAIS SAMIA AWATEMBELEA MAWAZIRI WAKUU WASTAAFU, MZEE MALECELA, MIZENGO PINDA DODOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here