Home SPORTS WAZIRI MCHENGERWA ATEMBELEA BASATA, COSOTA NA BODI YA FILAMU

WAZIRI MCHENGERWA ATEMBELEA BASATA, COSOTA NA BODI YA FILAMU

DAR ES SALAAM.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa , leo Januari 17, 2022, amefanya ziara ya kikazi kutembelea taasisi za Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika taasisi za Bodi ya Filamu, Baraza la Sanaa (BASATA) na Taasisi ya Hakimiliki (COSOTA), Waziri Mchengerwa amesisitiza huduma bora na utetezi wa haki na maslahi ya wasanii.

Aidha, ameziagiza taasisi hizo kuwekeza katika ubunifu ili ziweze kutoa huduma nzuri kwa wadau wa tasnia hizo za sanaa.

Katika ziara hiyo aliongozana na Naibu Waziri, Mhe. Pauline Gekul, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi na Naibu Katibu Mkuu Said Yakub.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here