Home SPORTS WAZIRI MCHENGERWA ATEMBELEA BASATA, COSOTA NA BODI YA FILAMU

WAZIRI MCHENGERWA ATEMBELEA BASATA, COSOTA NA BODI YA FILAMU

DAR ES SALAAM.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa , leo Januari 17, 2022, amefanya ziara ya kikazi kutembelea taasisi za Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika taasisi za Bodi ya Filamu, Baraza la Sanaa (BASATA) na Taasisi ya Hakimiliki (COSOTA), Waziri Mchengerwa amesisitiza huduma bora na utetezi wa haki na maslahi ya wasanii.

Aidha, ameziagiza taasisi hizo kuwekeza katika ubunifu ili ziweze kutoa huduma nzuri kwa wadau wa tasnia hizo za sanaa.

Katika ziara hiyo aliongozana na Naibu Waziri, Mhe. Pauline Gekul, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi na Naibu Katibu Mkuu Said Yakub.

Previous articleVIONGOZI WA DINI NA KIMILA MKOA WA KILIMANJARO WAOMBWA KUTOA ELIMU YA UVIKO-19 NA HAMASA YA CHANJO.
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.NNE JANUARI 18-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here