Home BUSINESS WAZIRI DKT. NDUMBARO APEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA NCHINI MAREKANI, KUSHIRIKI MKUTANO WA...

WAZIRI DKT. NDUMBARO APEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA NCHINI MAREKANI, KUSHIRIKI MKUTANO WA 50 WA UWINDAJI KITALII


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Kanza mara baada ya kuwasili nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention) ulioandaliwa na Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza akisalimiana na Afisa Mkuu wa Wanyamapori, Segolini Tarimo mara baada ya kuwasili nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention) ulioandaliwa na Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa.

Kaimu Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Elsie Kanza mara baada ya kuwasili nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention) ulioandaliwa na Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa.

NA: MWANDISHI WETU MAALUM, NEW YORK,MAREKANI.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amewasili Jijini hapa New York, Marekani leo  tarehe 18 Januari  2022 kwa ajili ya kushiriki mkutano wa  50 wa mwaka  wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention) ulioandaliwa na Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa.

Mkutano huo unaotarajiwa kuanza kesho tarehe 19 Januari, 2022 katika Jiji la  Las Vegas, Nevada nchini Marekani umelenga  kuwakutanisha  watunga sera na wafanya maamuzi katika ngazi  za juu kutoka nchi  mbalimbali duniani kuweza kujadili masuala ya kisera katika kuendeleza sekta ya uwindaji.

Katika Mkutano huo, 

Dkt. Ndumbaro anatarajia pia kunadi fursa za uwekezaji za uwindaji wa kitalii zilizopo nchini  Tanzania kwa lengo la kuwawezesha Matajiri wakubwa duniani kuchangamkia uwekezaji huo uliopo nchini Tanzania

Aidha,  katika mkutano huo Tanzania ni mshiriki muhimu ikizingatiwa kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazoongoza duniani katika uhifadhi wa wanyamapori na uwindaji, Hivyo kupitia mkutano huo Tanzania itaweza kuongeza uelewa zaidi katika masuala ya kisera na maamuzi katika kuendeleza sekta ya uwindaji wa kitalii nchini

Kando ya mkutano huo, katika hatua nyingine,  Dkt. Ndumbaro atapata fursa ya kufanya mazungumzo na Wadau mbalimbali wa masuala ya utalii waliopo hapa Marekani ikiwa ni nafasi adimu ya kuwavutia kwenda  kuwekeza nchini Tanzania. 

Katika msafara huo, Waziri Dkt. Ndumbaro ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TAWA, Meja Jenerali, Hamis Semfuko, Kaimu Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi,

Wengine ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TAWA, Lulu Ng’wanakilala pamoja na Afisa Mhifadhi Mkuu wa Wanyamapori wa kutoka TAWA, Segolin Tarimo

Waziri Ndumbaro pamoja na ujumbe wake wamepokelewa  na Mwenyeji wa  Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Kanza

Mwisho.





Previous articleBORESHENI HUDUMA ZA TIBA KWENYE HOSPITALI ZA RUFAA NA MIKOA: WAZIRI UMMY
Next articleKIJAZI AMKABIDHI RASMI OFISI MWAKILEMA, AWAASA WAFANYAKAZI WA TANAPA KUIMARISHA MSHIKAMANO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here