Home LOCAL BORESHENI HUDUMA ZA TIBA KWENYE HOSPITALI ZA RUFAA NA MIKOA: WAZIRI UMMY

BORESHENI HUDUMA ZA TIBA KWENYE HOSPITALI ZA RUFAA NA MIKOA: WAZIRI UMMY

Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu akiongea na watumishi wa Idara ya tiba ikiwa ni mwendelezo wa kuongeza na Idara mbalimbali Kwenye wizara hiyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi akiongea na watumishi wa Idara ya tiba.

Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Aifello Sichalwe akiongea Jambo wakati wa kikao kazi hicho.

Waziri Ummy Mwalimu Akizungumzia na watumishi.

Na: WA-Dodoma.
Hospitali za rufaa za mikoa nchini zimetakiwa kuboresha huduma za afya pamoja na kuwa na mawazo mapana katika kuboreshaji wa miundombinu ya hospitali hizo ili kuweza kuisaidia na kuipunguzia mzigo hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiongea na wafanyakazi wa idara ya tiba ikiwa ni mwendelezo wa kukutana na kufanya mapitio ya idara mbalimbali zilizopo kwenye wizara hiyo.

Mhe. Ummy amesema ili kuonesha kweli idara ya tiba ndio inayobeba wizara hiyo hamna budi kuboresha huduma hizo ili zilingane na mahitaji ya wananchi kwani wananchi wanaziamini hospitali za umma.

“tunatakiwa kuhakikisha utoaji wa huduma za afya ni mzuri, hivyo ni wakati wa kuangalia changamoto na kuziboresha ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi ambao wanafika kwenye vituo vyetu kupata huduma“ amesema Mhe. Ummy.

Aidha, Waziri huyo ameitaka idara hiyo kufanya upya mapitio ya miongozo ya utoaji huduma ili kufanya huduma zinazotolewa kuanzia ngazi ya zahanati hadi Taifa zinakuwa bora na zenye manufaa kwa wananchi vilevile miongozo hiyo iweze kuunganisha vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Hata hivyo Waziri Ummy amewataka watumishi wa idara hiyo kufanya kazi kama timu na endapo kuna changamoto ni vyema zikajadiliwa kwa pamoja ili kwenda kwa pamoja katika kuboresha huduma za afya nchini.
Previous articleTANZANIA PEACE FOUNDATION YASEMA MAZITO YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Next articleWAZIRI DKT. NDUMBARO APEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA NCHINI MAREKANI, KUSHIRIKI MKUTANO WA 50 WA UWINDAJI KITALII
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here