Home LOCAL TAARIFA KAMILI JUU YA AJALI ILIYOHUSISHA WAANDISHI WA HABARI MWANZA

TAARIFA KAMILI JUU YA AJALI ILIYOHUSISHA WAANDISHI WA HABARI MWANZA

Ndugu waandishi wa habari na wadau wa habari , asubuhi ya leo tuliwataarifu taarifa ya awali juu ya ajali ya waandishi wenzetu wa Mkoa wa Mwanza.

Baada ya kufika kwenye Zahanati ya Busenga nilipewa jukumu la kuwataambua  marehemu.

Waliofariki ni 

1.Husna Milanzi – ITV

2.Johari Shani – Uhuru Digital

3.Antony Chuwa – Habari leo Digital 

4.Abel Ngapenda – Afisa Habari ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza

5.Steven Msengi – Afisa Habari Ukerewe.

Majeruhi.

1.Tunu Heman – Freelancer

2 Vany Charles  – Icon TV

Kwa sasa tupo njiani na miili ya wapendwa wetu kuelekea hospitali ya Mkoa ya Seketoure Mwanza.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Simiyu chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa magari yote mawili na amethibitisha vifo hivyo.

Taarifa nyingine za uratibu wasibu wa msiba  tutawajuza.

Mwanza press club tumepokea kwa masikitiko makubwa msiba huu.

Kazi ya Bwana haina makosa, jina.lake lihidimiwe.

 Edwin Soko

 Mwenyekiti 

 Mwanza Press Club

 11.01.2022

Previous articleRAIS SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA NGUO CHA BASRA TEXTILE ZANZIBAR
Next articleHABARI KUU MAGAZETI YA LEO J.TANO JANUARI 12-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here