Home SPORTS SIMBA SC YAITIA ADAMU DAR CITY, YAIPIGA GOLI 6-0 BILA HURUMA

SIMBA SC YAITIA ADAMU DAR CITY, YAIPIGA GOLI 6-0 BILA HURUMA


Na: Mwandishi wetu, DAR.
Timu ya wekundu wa msimbazi Simba SC imefanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora ya  Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC), kwa kuitia hadabu bila huruma timu ya Dar City kwa kuichapa jumla ya bao 6 – 0 katika  Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yamefungwa na Meddie Kagere , Clatous Chama, Rally Bwalya, Pascal Wawa na Chris Mugalu ambaye alimalizia kazi.

Aidha Katika mchezo huo timu ya Simba ilionyesha Kandanda safi na kumiliki Mpira Katika vipindi vyote viwili ambapo mpaka mwamuzi wa mchezo huo anapuliza kipyenga cha mwisho Simba walikuwa wakimilki Mpira kwa asilimia 79.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here