Home SPORTS RANI SANITARY PADS YAPANDISHA MZUKA TANZANITE

RANI SANITARY PADS YAPANDISHA MZUKA TANZANITE

NA: MWANDISHI WETU, Zanzibar.

WASAMBAZAJI na wauzaji wa Rani Sanitary Pads (Taulo za kike) wametoa taulo hizo kwa kikosi cha timu ya taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) kinachojiandaa na mchezo wake dhidi ya Ethiopia Jumapili. 

Kikosi hicho kilichoweka kambi Zanzibar kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Amaan visiwani humo, ukiwa mchezo wa kutafuta nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia litakalochezwa nchini  Costarica. 

Muwakilishi wa Rani Sanitary Pads Mawi Zahor aliyeko visiwani humo alisema wameamua kuifuata kambini timu hiyo na kuwapa taulo hizo ili kuwaongezea hamasa ya mchezo huo.

Mawi aliongeza kuwa anaamini Tanzanite itashinda pambano hilo kutokana na maandalizi mazuri na kambi tulivu.

Tumekuwa wadau wakubwa wa soka la Wanawake nchini, ndiyo maana tumeona tuje hadi huku (Zanzibar) kuungana na hawa vijana wetu katika maandalizi ya mchezo huo wa Jumapili. 

“Tunaamini kwa tulichokitoa kitakuwa kizuri maana timu ya taifa inatakiwa kutumia taulo ambazo ni bora” Mawi.

Rani Sanitary Pads ambao ni mdhamini mweza wa ligi ya Wanawake wamekuwa na utaratibu wa kutoa taulo hizo kwa kikosi hicho na vikosi mbalimbali za timu ya Taifa. 

Ends.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here