Home BUSINESS NAIBU WAZIRI MARY MASANJA AWATAKA WAHITIMU CHUO CHA TAIFA CHA UTALII KUCHANGAMKIA...

NAIBU WAZIRI MARY MASANJA AWATAKA WAHITIMU CHUO CHA TAIFA CHA UTALII KUCHANGAMKIA FURSA ZA KUJIAJIRI


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Mary Masanja (Mb). akizungumza wakati wa Maafali ya 19 ya Chuo Cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo Januari 21,2022 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Utalii Philip Chitonga akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi kwenye Maafali hayo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt. Shogo Mlozi akitoa Salamu za utangulizi mara baada ya kuundwa rasmi kwa Maafali leo Januari 21,2021 Jijini Dar es Salaam.

Kikundi cha ngoma za asili cha Kusini Culture Group kikitumbuiza kwenye Maafali hayo. (PICHA  ZOTE NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Mary Masanja (Mb) amewataka wahitimu wa katika Sekta ya Utalii nchini kuzitumia fursa zilizopo kwenye Sekta hiyo ili kujiajiri wenyewe.


Mheshimiwa Masanja ameyasema hayo kwenye Maafali ya 19 ya Chuo cha Taifa cha Utalii yaliyofanyika leo Januari 21,2022 Jijini Dar es Salaam.


Amesema kuwa kwenye Sekta ya Utalii zipo fursa nyingi zinazopaswa kufikiwa nakwamba anaamini kuwa maarifa waliyopata wahitimu hao wanaweza kuzifikia fursa hizo na kuzianyia kazi.


“Ndugu wahitimu niwaombe sana mkaoneshe ujuzi na maarifa mliyoyapata kwa vitendo na bidii ya kazi ili kuleta tija kwenye kazi huku mkiziendea fursa zilizopo na kuzifanyiakazi, kwani kwa kufanya hivyo mtaweza kujiajiri wenyewe na kuendesha maisha yenu” amesema Mhe. Masanja.


Amebainisha kuwa Sekta hiyo kwa sasa imeendelea kuimarika kutokana na kuwepo kwa janga la uviko 19 na kwamba mafanikio hayo yametokana na jitihada za Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mpango wa kukabiliana na janga hilo ikiwemo mpango wa Chanjo.


“Ndugu wahitimu Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya jitihada kubwa kushughulikia janga la Uviko 19 ikiwemo mpango wa Chanjo, mpango huo umeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa maambukizi mapya ya Uviko 19 na hivyo kusaidia kuendelea kuimarika kwa Sekta ya Utalii” Ameongeza Mhe. Masanja.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utalii Philip Chitonga amesema kuwa Chuo hicho kimeendelea kuwa na tija kubwa kutokana na vijana wengi kuona fursa ya kujiajiri wenyewe baada ya kuhitimu masomo yao na kupata ujuzi na maarifa katika Sekta hiyo.


“Chuo kimeendelea na jitihada za kuboresha utendaji kazi wake ili kuzidi kuwasaidia wahitimu wake, ujuzi na mbinu bora zaidi za kutambua fursa zilizopo kwenye Sekta ya Utalii na kuzifanyiakazi kazi” Amesema Chitonga.


Awali akizungumza wakati wa kutoa Salamu za utangulizi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dkt. Shogo Mlozi amesema kuwa Chuo hicho kimeendelea kujenga mahusiano mazuri na Taasisi nyingine na wadau mbalimbali katika Sekta hiyo vikiwemo vyuo vinavyotoa elimu ya Utalii ndani na nje ya nchi.


“Chuo kumekuwa na mafanikio makubwa Katika kuongeza mafunzo ya kozi mbalimbali ili kutoa fursa kwa vijana wa kitanzania kupata maarifa na ujuzi katika Sekta ya Utalii” Amesema Dkt. Shogo.


Chuo cha Taifa cha Utalii ni Chuo pekee cha Umma kilichopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii chenye dhamana ya kutoa mafunzo ya ukarimu na Utali, pia kutoa huduma za ushauri kitaalam na kufanya tafiti mbalimbali katika fani ya ukarimu na Utalii.

Mwisho.


Zifuatazo ni Picha za matukio mbalimbali Katika Maafali hayo.




Previous articleKONGANI YA VIWANDA KUJENGWA DODOMA
Next articleRANI SANITARY PADS YAPANDISHA MZUKA TANZANITE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here