Na: Heri Shaaban.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema anatarajia kufanya ziara Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa Wilayani Ilala.
Rais Samia Suluhu Hassan aliyasema hayo wakati wa siku yake ya kuzaliwa alipokuwa akizungumza na simu moja kwa moja na Wanafunzi wa Benjamini Mkapa katika sherehe yake ya kuzaliwa kupitia Televisheni ya Taifa TBC 1.
“Napongeza uongozi wa Shule ya Sekondari Benjamini Mkapa kwa kuniandalia siku hii yangu ya kuzaliwa leo nina ahidi nitakapokuja Dar es Salam nitafanya ziara shule yenu ya Benjamini Mkapa “alisema Rais Samia Suluhu.
Rais Samia alimpongeza Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia Proresa Adolf Mkenda, ambaye alimwakilisha katika Badhiday hiyo iliyofanyika Benjamini Mkapa.
Akizungumzia changamoto za shule ya Benjamini Mkapa Rais Samia alisema serikali itazitatua changamoto zote za shule hiyo.
Akizungumzia Sekta ya Elimu alisema Sekta ya Elimu ina mambo mengi mikakati yake serikali itaendelea na mikakati ya kujenga shule za msingi kuongeza madarasa nchini nzima.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda aliwataka Watanzania tuliombee Taifa letu
Nchi yetu aina ubaguzi wowote kuanzia Sekta ya Elimu wanafunzi wa rika zote wanapatiwa Elimu.
Waziri wa Elimu alisema mwaka 2022 serikali imewapeleka shule ya sekondari jumla ya Wanafunzi 900,000 nchini nzima.
Alisema baadhi ya mikakati ambayo ametekeleza Rais katika sekta ya Elimu amejenga vyuo 25 vya VETA nchini nzima pamoja na madarasa ya shule za sekondari.
Mkuu wa Shule ya Benjamini Mkapa Deo Joseph alisema shule hiyo ina jumla ya Wanafunzi 1635 wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha sita ambapo Wanawake 719 wa kiume 916 .
Mwalimu Deo alisema shule ya Benjamini inatoa Elimu Jumuishi yaani ina wanafunzi wasio na majitaji Maalum na walio na mahitaji maalum.
Akielezea changamoto za shule alisema shule ya Benjamin Mkapa ina changamoto ya chumba cha kupimia ulemavu wa masikio (Viziwi) gari la Wagonjwa kwa ajili kurahishisha huduma kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa kuwa ni changamoto wakati wakiumwa pamoja na ukumbi wa maktaba na mikutano.
Mwisho