Home LOCAL RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA SHULE BENJAMINI MKAPA

RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA SHULE BENJAMINI MKAPA


Na: Heri Shaaban.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema anatarajia kufanya ziara Shule ya  Sekondari Benjamini Mkapa   Wilayani  Ilala. 

Rais Samia Suluhu Hassan aliyasema hayo wakati  wa siku yake ya kuzaliwa alipokuwa  akizungumza na simu moja kwa moja na Wanafunzi wa Benjamini Mkapa katika sherehe yake ya kuzaliwa kupitia Televisheni ya Taifa TBC 1.

Napongeza uongozi wa Shule ya  Sekondari Benjamini Mkapa kwa kuniandalia siku hii yangu ya kuzaliwa leo  nina ahidi nitakapokuja Dar es Salam nitafanya ziara shule yenu ya Benjamini Mkapa “alisema Rais Samia Suluhu. 

Rais Samia alimpongeza Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia Proresa Adolf Mkenda, ambaye alimwakilisha katika Badhiday hiyo iliyofanyika Benjamini Mkapa. 

Akizungumzia changamoto za shule ya Benjamini Mkapa  Rais Samia alisema serikali itazitatua changamoto zote za shule hiyo. 

Akizungumzia Sekta ya Elimu alisema Sekta ya Elimu ina mambo mengi mikakati yake serikali itaendelea na mikakati  ya kujenga shule za msingi kuongeza madarasa nchini nzima. 

Kwa upande wake Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa  Adolf Mkenda aliwataka Watanzania tuliombee Taifa letu  
Nchi yetu aina ubaguzi wowote kuanzia Sekta ya Elimu wanafunzi wa rika zote wanapatiwa Elimu.

Waziri wa Elimu alisema mwaka 2022 serikali imewapeleka shule ya sekondari jumla ya Wanafunzi 900,000 nchini nzima. 

Alisema baadhi ya mikakati ambayo ametekeleza Rais katika sekta ya Elimu  amejenga vyuo 25 vya VETA nchini  nzima  pamoja na  madarasa ya shule za sekondari.

Mkuu wa Shule ya Benjamini Mkapa  Deo Joseph alisema   shule hiyo ina jumla ya Wanafunzi 1635 wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha sita  ambapo Wanawake 719 wa kiume 916 .

Mwalimu Deo alisema shule ya Benjamini inatoa Elimu Jumuishi yaani ina wanafunzi wasio na majitaji Maalum na walio na mahitaji maalum. 

Akielezea changamoto za shule alisema shule ya Benjamin Mkapa ina changamoto ya chumba cha kupimia ulemavu wa masikio (Viziwi) gari la Wagonjwa kwa ajili kurahishisha huduma kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa kuwa ni changamoto wakati wakiumwa pamoja na ukumbi wa maktaba na mikutano. 

Mwisho
Previous articleKAMATI ZA UKIMWI ZAAGIZWA KUKUTANA NA KUSHIRIKISHA WADAU MBALIMBALI
Next articleMITINDO YA MARTIN KADINDA MPAKA MBUGANI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here