Home SPORTS PABLO: KIKOSI KIKO IMARA DHIDI YA MTIBWA SUGAR

PABLO: KIKOSI KIKO IMARA DHIDI YA MTIBWA SUGAR

Na: Stella KESSY.

Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba amesema kuwa timu yake leo imeanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa jumamosi dhidi ya Mtibwa.

Ameyasema hayo leo kabla ya kikosi kuanza safari ya kuelekea makoani Morogoro kwa ajili ya mtanange huo.

“Baada ya timu kutoka jijini Mbeya wachezji wamepata siku mbili za kufanya mazoezi na kesho tutafanya ya mwisho kabla ya mchezo wa junamosi nafahamu mchezo utakuwa mgumu lakini benchi la ufundi pamoja na wachezaji wapo tayari kuhakikisha kila mmoja anatimiza majukumu yake ili ushindi uapatikane” amesema.

Pia ameongeza kuwa “jambo zuri ni kwamba tumepata muda wa kufanya mazoezi katika mechi iliyopita jambo hilo halikuwepo, pia kesho tutapata muda wa kufanya tena zoezi la mwisho kabla ua mchezo wetu na Mtibwa”

Aidha pabloa amekiri mchezo kuwa mgumu kutokana na kusafiri mfululizo kutoka zanzibar Mbeya kisha Morogoro lakini wamejipanga na wapo tayri kupambana kuhakikisha wanashinda.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here