Home SPORTS BAHATI ATUA BIASHARA UNITED

BAHATI ATUA BIASHARA UNITED


Na: Mwandishi wetu.

BIASHARA United imemtambulisha rasmi Vivier Bahati kuwa kocha mkuu wa timu hiyo na tayari ameanza kazi rasmi kuinoa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara.

Bahati alikuwa anainoa timu ya Azam FC mkataba wake ulivunjwa kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo na waliondoka pamoja na Kocha Mkuu, George Lwandamina.

Anachukua mikoba ya Patrick Odhiambo ambaye amebwaga manyanga hivi karibuni ndani ya timu hiyo inayotumia Uwanja wa Karume,Mara.

Vivier Bahati amepewa dili la miezi sita kwa ajili ya kuinoa timu hiyo iliyo nafasi ya 15 na pointi 10.

Mchezo wake ujao ni dhidi ya Geita Gold na utachezwa Uwanja wa Karume itakuwa ni Januari 22.

Previous articlePABLO: KIKOSI KIKO IMARA DHIDI YA MTIBWA SUGAR
Next articleHABARI KUU MAGAZETI YA IJUMAA JANUARI 21-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here