Home LOCAL MHE UMMY MWALIMU AKAGUA UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI ILIYOPO SARUJI,...

MHE UMMY MWALIMU AKAGUA UJENZI WA SHULE MPYA YA SEKONDARI ILIYOPO SARUJI, KATA YA MAWENI

Awapongeza Mkuu wa Wilaya na Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kazi nzuri

Viongozi waomba iwe Shule ya Wasichana na iitwe Ummy Mwalimu Secondary School.

TANGA

Mbunge wa Tanga Mjini na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe Ummy Mwalimu  leo tarehe 7/01/2022 amekagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari iliyopo Saruji, Kata ya Maweni Jijini Tanga ambapo  madarasa 14  yamejengwa kwa pesa za UVIKO kiasi cha  shilingi milioni 280. Mhe Ummy ameridhishwa na ujenzi huo. Aidha amewapongeza Viongozi na Watendaji wa Jiji la Tanga kwa kukamilisha ujenzi huo kwa wakati. 

Pia amefurahishwa na hatua ya Jiji la Tanga kutumia mapato yake ya ndani kujenga matundu ya vyoo 12 kwa ajili ya wanafunzi na maabara 1 ya masomo ya Sayansi. 

Mhe Ummy amewataka  Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuiga mfano wa Jiji la Tanga na kuhakikisha wanatumia mapato ya ndani kujenga matundu ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi ili kuendana na ongezeko la madarasa ya Samia yaliyojengwa kwa fedha za UVIKO. 

Wakiongea kabla ya kumkaribisha Mhe Waziri, Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe Hashim Mgandilwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Maweni Ndugu Mpokigwe Anyitike wamempongeza *Rais Rais Samia Suluhu Hassan*kwa kutoa fedha za ujenzi wa madarasa 54 kwa mpigo kwa ajili ya wanafunzi wa Jiji la Tanga jambo ambalo halijahi kutokea! Pia wamemshukuru Mhe. Ummy kwa kazi nzuri ya kumsaidia Rais Samia na kazi nzuri anazozifanya kutatua kero za wana Tanga. Aidha wameomba Shule hiyo iwe ya Wasichana na iitwe Ummy Mwalimu Girls Secondary School.

Katika ziara hiyo, Mhe Ummy aliambatana na Katibu wa CCM Wilaya ya Tanga Ndg. Twalibu Bellege, Diwani Viti Maalum, Mhe Mariamu Ng’azi na wakuu wa idara na Watumishi wa Halmashauri wa Jiji la Tanga.

Imetolewa na;

Ofisi ya Mbunge,

Jimbo la Tanga Mjini 

07/01/2022.

Previous articleYANGA YATOKA SARE YA 2-2 NA KMKM MAPINDUZI CUP
Next articleRAIS MHE,.DK.HUSSEIN MWINYI AFUNGUA MADARASA MAPYA SITA YA SKULI YA MSINGI SEBLENI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here