Home BUSINESS FEDHA ZA REGROW KUBORESHA HIFADHI YA TAIFA MIKUMI

FEDHA ZA REGROW KUBORESHA HIFADHI YA TAIFA MIKUMI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe.Mary Masanja (Mb) akisalimiana na watumishi wa Hifadhi ya Taifa Mikumi alipotembelea Hifadhi hiyo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa mradi wa REGROW Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akikagua gwaride alipotembelea Hifadhi ya Taifa Mikumi kwa lengo la kukagua utekelezaji wa mradi wa REGROW Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na watumishi wa Hifadhi ya Taifa Mikumi kuhusu Mradi wa Kusimamia na Kuendeleza Utalii Nyanda za Juu Kusini (REGROW) katika kikao kilichofanyika Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Denis Londo akitoka mapendelezo ya namna ya kuiboresha Hifadhi ya Taifa Mikumi katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe.Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) na watumishi wa Hifadhi ya Taifa Mikumi kilichofanyika Januari 24,2022 Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.


Baadhi ya Maafisa Uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa Mikumi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) alipofanya kikao kwa ajili ya kujua Maendeleo ya Utekelezaji wa Mradi wa REGROW pamoja na kutatua changamoto zinazoikabili Hifadhi ya Taifa Mikumi Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.
MOROGORO.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema Hifadhi ya Taifa Mikumi ni miongoni mwa hifadhi iliyotengewa fedha za Mradi wa Kusimamia  na Kuendeleza Utalii Nyanda za Juu Kusini (REGROW) hivyo inatarajiwa kuwa na miradi ya kimkakati itakayosaidia kuongeza idadi ya watalii katika eneo hilo.

Amesema hayo Januari 24 Mwaka huu alipotembelea hifadhi hiyo katika Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro leo.

Mhe. Masanja ameongeza kuwa mradi wa REGROW umetenga kiasi cha dola za kimarekani milioni 69 zitakazogawanywa kwenye Hifadhi za Taifa za Mikumi, Udzungwa na Ruaha na Nyerere imetengewa Dola za kimarekani milioni 37.7.

“Fedha za REGROW zitatumika kununua mitambo, vifaa vya doria, vitendea kazi vya ofisi, kuboresha maeneo mbalimbali kama kujenga hostel, picnic sites, bandaz, camp sites, rest houses, ranger posts na viwanja vya ndege.

Aidha, Mhe. Masanja amewahimiza watanzania kutembelea eneo hilo kwa ajili ya kutalii na pia kuwekeza ndani ya hifadhi hiyo.

Previous articleTET YAWASILISHA MADA YA UBORESHAJI WA MITAALA YA ELIMU KWA UMOJA WA WAKUU WA SHULE ZA KIKRISTO ‘CSSC’
Next articleTAKUKURU ARUSHA YATOA TAHADHARI UWEPO MATAPELI WANAODAI NI FAOFISA WAO, YAFUATILIA SHILINGI BILIONI 12.6 FDHA ZA CHANJO UVIKO-19 NA MRADI EP4R.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here