Home LOCAL COSTECH YAWAKUTANISHA WATAFITI JIJINI DODOMA

COSTECH YAWAKUTANISHA WATAFITI JIJINI DODOMA


Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi ,Teknlojia na Ubunifu (COSTECH) Dkt.Wilbert Manyilizu,akizungumza wakati wa semina kwa wakurugenzi wa Sera na Mipango iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi ,Teknlojia na Ubunifu (COSTECH) iliyofanyika leo Januari 6,2022 jijini Dodoma.


Kaimu Kamishna Mipango ya Kitaifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Royal Lyanga,akizungumza wakati wa semina kwa wakurugenzi wa Sera na Mipango iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi ,Teknlojia na Ubunifu (COSTECH) iliyofanyika leo Januari 6,2022 jijini Dodoma.


Afisa utafiti Mwandamizi Tume ya Sayansi ,Teknlojia na Ubunifu (COSTECH) Merchades Method,akielezea lengo la semina kwa wakurugenzi wa Sera na Mipango iliyoandaliwa na COSTECH iliyofanyika leo Januari 6,2022 jijini Dodoma.

 Baadhi ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa semina kwa wakurugenzi wa Sera na Mipango  iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi ,Teknlojia na Ubunifu (COSTECH) iliyofanyika leo Januari 6,2022 jijini Dodoma.


Mtafiti kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof.Goodluck Makundi,akitoa mawasilisho kuhusu magonjwa yasiyoambukiza wakati wa semina kwa wakurugenzi wa Sera na Mipango iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi ,Teknlojia na Ubunifu (COSTECH) iliyofanyika leo Januari 6,2022 jijini Dodoma.



Kaimu Kamishna Mipango ya Kitaifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Royal Lyanga,akichangia mada wakati wa semina kwa wakurugenzi wa Sera na Mipango iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi ,Teknlojia na Ubunifu (COSTECH) iliyofanyika leo Januari 6,2022 jijini Dodoma.


Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw.Joel Mangi,akichangia mada wakati wa semina kwa wakurugenzi wa Sera na Mipango iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi ,Teknlojia na Ubunifu (COSTECH) iliyofanyika leo Januari 6,2022 jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi ,Teknlojia na Ubunifu (COSTECH) Dkt.Wilbert Manyilizu,akiwa katika picha ya pamoja  wakati wa semina kwa wakurugenzi wa Sera na Mipango iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi ,Teknlojia na Ubunifu (COSTECH) iliyofanyika leo Januari 6,2022 jijini Dodoma.

DODOMA.

WATAFITI wamependekeza ili kukabiliana na magonjwa yasiyoyakuambukiza nchini sheria na kanuni zilizopo ziimarishwe,bidhaa za tumbaku ziongezewe kodi, na  kutumia maafisa maendeleo ya jamii kuelimisha watu katika ngazi tofauti tofauti.

Akizungumza leo,Januari 6,2022,Jijini Dodoma, wakati wa semina kwa wakurugenzi wa Sera na Mipango iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi ,Teknlojia na Ubunifu (COSTECH) ambao ulikuwa ni kwa ajili ya kutoa ripoti ya matokeo ya utafiti katika  sekta ya afya uliofanywa na  watafiti mbalimbali hapa nchini, Prof. Goodluck Makundi amesema, magonjwa yasiyo ya kuambukiza hapa nchini bado ni changamoto.


Amesema matokeo ya utafiti wao umeonyesha,pamoja na mambo mengine kuna upungufu wa fedha za kugharamia magonjwa hayo ambapo asilimia 7.8 ya matumizi ya sekta hiyo ndio hutumika ikilinganisha na tatizo  la asilimia 41.


Akitoa mapendekezo katika sekta ya afya amesema ,inahitaji uratibu wa hali ya juu kwa kutumia ofisi mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Rais Tamisemi,lakini pia sheria na kanuni zilizopo dhidi ya mapambano ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ziimarishwe.


“Mfano bidhaa za mazao ya tumbaku ziongezwe  kodi pamoja na kupiga marufuku matangazo yake.”amesema.


Vilevile amesema  pendekezo lingine ni kuanza kuzungumzia elimu ya magonjwa haya katika ngazi  tofauti tofauti,pia yaingizwe kwenye mpango wa elimu ya afya mashuleni.


Profesa Makundi pia amesema  pendekezo lingine ni ,vyombo vya habari vikiwemo vya mitandao ya kijamii ,vilete  mabadiliko kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na magonjwa hayo.


“Social media(mitandao ya kijamii) inaweza kutumika ‘positively’ maana media ni eneo ambalo tukishirikiana vizuri linaweza kuleta matokeo chanya .”amesema.


Pia, amesema watafiti katika eneo hilo la afya wamependekeza kuwepo na uwekezaji zaidi huku akisema,kuna haja ya kutafiti zaidi na kuwekeza kwenye utafiti ili kutatua matatizo hayo lakini pia kuna haja ya kutumia maafisa maendeleo ya jamii kuelimisha watu katika ngazi tofauti tofauti.


“Viongozi wa dini wana  wajibu wa kuelezea angalau kwa dakika chache wawapo katika ibada zao huku akisema,hii itasaidia waumini kupata uelewa juu ya magonjwa haya katika maeneo tofauti tifauti a kuwapa uelewa wa kutosha.


“Kwa hiyo tunaona kuna haja ya kutumia majukwaa tofauti tofauti katika kupambana na magonjwa haya,lakini pia  kila  mtu ahusike katika kuchukua hatua ikiwemo kufanya mazoezi,pia taasisi mbalimbali zikiwemo shule shule nazo zina jukumu la kuhamasisha mazoezi..,pia vyakula vyakula nyumbani vizingatie suala la lishe .”amesema Profesa Makundi.

Kuhusiana na ripoti ya Mwaka  2020 ya Takwimu za Kamisheni ya Umasikini na Magonjwa amesema  imeonyesha kuwa asilimia 41 ya utafiti uliofanyika Tanzania katika kipindi hicho ,ni  ya magonjwa yasiyoambukiza na majeruhi.
Amesema utafiti huo umeonyesha kuwa mwaka 2020 Tanzania ilitumia dola milioni 700  kugharamia katika kukinga na kutibu magonjwa hayo.


“Kuna ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa nchini Tanzania na kufikia vifo,ongezeko hili ni mara mbili ya hali ilivyokuwepo mwaka 2015,hali hii inasababisha nguvu kuelekezwa zaidi katika  kutibu kuliko kukinga ,na ni ghali  kutibu kuliko kukinga.”amesema.


Prof. Makundi amesema  tatizo  hilo haliwakumbi watu wazima na wazee tu bali hata vijana na watoto wanakumbwa huku akisema linachangiwa sana na  mabadiliko ya mtindo wa maisha na lishe.


Aidha amesema,hilo ni tatizo mtambuka linahusisha sekta mbalimbali.
“Ni changamoto kubwa hapa nchini kwa magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza ,magonjwa haya ni pamoja na moyo,shinikizo la damu,saratani mbalimbali pamoja na magonjwa ya mfumo wa hewa,”amesema.


Prof. Goodluck amevitaja  baadhi ya vitu vinavyosababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza kuwa ni pamoja na matumizi ya tumbaku,kutofanya mazoezi,ulaji vyakula usiozingatia lishe bora na matumizi ya  pombe kupita kiasi.
Amesema,Shirika la Afya Duniani linasema,mambo hayo yanachangia kwa asilimia 80 ya tatizo hilo duniani.

Awali akifungua semina hiyo iliyoandaliwa na Tume ya Sayansi ,Teknlojia na Ubunifu (COSTECH) mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt.Wilbert Manyilizu amesema lengo la warsha  hiyo ni kuwashirikisha Wadau wakuu wa matokeo ya tafiti za kisayansi na  Teknolojia ili waweze kuwasilisha na kutoa matokeo ya tafiti zao.

Amesema ,Costech iliwaita watafiti katika Sekta nne za awali ambazo ni sekta ya Afya,Kilimo,maliasili na mifugo  ili wawasilishe tafiti zao ambazo hufanyiwa kazi na Tume hiyo ambayo ndio yenye dhamana ya kuishauri Serikali katika masuala ya sayansi na teknolojia.


Aidha amesema,lengo la kuanzishwa kwa Tume hiyo ni  kuishauri Serikali katika masuala ya sayanasi na Teknolojia na ubunifu huku akisema,jukumu kubwa la COSTECH ni kuratibu na kuhamasisha mambo ya utafiti na ubunifu ambapo katika jukumu hilo pia kuna majukumu mengine.


Ameyataja majukumu hayo kuwa ni pamoja na kusimamaia Menejimenti ya maarifa yanayopatikana katika ubunifu na utafiti na baadae kusambaza kwa Wadau huku akisema, michakato yote ya kuwatambua na kuwawezeaha wabunifu ni jukumu lao.
Aidha amesema,jukumu lingine  la Tume hiyo ni kuhabarisha Wanachi na Wadau mbalimbali kwa kukusanya na kusambaza taarifa za sayansi  na ubunifu wa wananchi pamoja na kusambaza vijarida.

Credit – Fullshangwe Blog.

Previous articleMHE. UMMY NDERIANANGA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA MKOA WA KUSINI UNGUJA
Next articleHITIMANA KOCHA MPYA KMC
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here