Home LOCAL BORESHENI MADARASA YA ZAMANI ILI YAFANANE NA YALE YA UVIKO –...

BORESHENI MADARASA YA ZAMANI ILI YAFANANE NA YALE YA UVIKO – 19 UBUNGO ” KAMATI YA SIASA MKOA DSM

Yawataka Wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuondoa ziro Dsm

Yaitaka Ubungo kuongeza zaidi walimu wa kuwafundisha Wanafunzi

Yapongeza Maono ya Rais Samia kutoa Fedha za Covid- 19″ Ubungo

DAR ES SALAAM.

Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dar es Salaam imeendelea na ziara yake katika Mkoa huo ambapo leo ilikuwa katika Wilaya ya Ubungo na  kuitaka  Wilaya hiyo kuboresha Madarasa yaliyojengwa zamani ili yafanane na yale ya Uviko-19 kufuatia utofauti Mkubwa kujitokeza Kati yao ambapo yale ya zamani kuonekana yamechakaa.

Hayo yamesemwa leo tarehe 19 Julai 2022 na Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Adam Ngalawa. Q”Kupitia mapato ya ndani endeleeni kuboresha Madarasa hayo ili nayo yafanane na ya Uviko-19″ . Adam Ngalawa

Aidha Kamati hiyo imewataka Wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato Cha kwanza kusoma kwa bidii kwani Elimu ndio Msingi wa maisha yao na itawafanya kuondoa ZIRO katika mithihani Yao.

Wakati huo huo Kamati imeitaka Wilaya hiyo kuongeza idadi ya walimu sehemu zote zenye upungufu wa Walimu ikibidi kutumia walimu kwa mkataba ambao wako mitaani na hawana ajira.

Hata hivyo Kamati imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi Cha Shilingi Bilioni 3  kwa Wilaya ya Ubungo ili kujenga Madarasa, matundu ya vyoo na Zahanati.

Kamati hiyo imetembelea Miradi ya Ujenzi wa Madarasa ya Sekondari, Ujenzi wa Daraja katika stendi ya Mabasi Kituo Cha Magufuli na Ukamilishaji wa Majengo Saba katika hospitali ya Wilaya ya Ubungo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here