Home SPORTS BMT LATOA ONYO KALI KWA KAMISHENI YA NGUMI ZA KULIPWA (TPBRC) KUMPA...

BMT LATOA ONYO KALI KWA KAMISHENI YA NGUMI ZA KULIPWA (TPBRC) KUMPA KIBALI BONDIA ALIYEFUNGIWA

 

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limetoa onyo kwa viongozi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC)  baada ya kumpa kibali bondia ambaye amefungiwa nchini kwao.

Akizungumza jana na Kaimu Mkuu Kitendo cha Uhusiano wa BMT,  Najah Bakari amesema kuwa onyo hilo ni kutokana na viongozi hao kumchezesha   bondia ambaye alikuwa amefungiwa nchini kwao Ghana.

“Makamu wa raisi Agapito Jambwale  na Katibu Mkuu Yahya Poli walitoa kibali cha bondia raia wa Ghana Richard Harrison kwenda kucheza pambano Novemba 03,mwaka jana nchini Urusi akiwa amefungiwa, “amesema .

Aidha baraza hilo limetoa onyo kali kwa promota wa ngumi za kulipwa hapa nchini Jay Msangi kwa kumwombea kibali bondia huyo ambaye amefungiwa.

“Baada ya kufanya uchunguzi wa suala hilo na kujiridhisha  kuwa ni kweli  bondia huyo alikuwa amefungiwa nchini kwake   kutokujihusisha na mchezo wa ngumi za kulipwa ,hivyo kutoa kibali kwa bondia aliyefungiwa nchini kwake ni kukiuka kanuni na taratibu na miongozo ya baraza pamoja na katiba ya TPBRC,,”amesema.

Baraza limewataka mapromota wa ngumi,mawakala na viongozi wa vyama vya michezo yote kuhakikisha kuwa wanazingatia taratibu ,miongozo kanuni na sheria zinazosimamia michezo nchini .

Amesema kuwa kwa sasa viongozi wanatakiwa kuwajibika kwa umakini katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuleta ustawi wa michezo nchini.

Previous articleHITIMANA KOCHA MPYA KMC
Next articleRAIS DKT.HUSSEIN MWINYI AFUNGUA MARIJANI RESORT& SPA PWANI MCHANGANI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here