Home SPORTS BAO LA MCHEZAJI HAMIS KIIZA LAPELEKA KILIO MSIMBAZI

BAO LA MCHEZAJI HAMIS KIIZA LAPELEKA KILIO MSIMBAZI


Na: Mwandishi wetu,KAGERA.

BAO pekee lililofungwa na Mchezaji wa Kagera Sugar Hamis Kiiza limetosha kupeleka kilio kwa klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliochezwa leo katika Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera, wachezaji wa timu ya Simba na Kagera wote walikuwa wanatumia mbinu,akili na maarifa katika kusakata kabumbu.

Wakati mchezo huo ukiendelea Simba ilionekana kuutawala mchezo kwa kiwango kikubwa lakini wachezaji wa Kagera walifanikiwa kudhibiti njia zote ambazo waliamini wasipokuwa  makini wanaweza kutoa nafasi kwa mpinzani.

Simba ambayo Katika mchezo wa leo iliingia uwanjani ikiwa na wachezaji wengi viungo na hakukua na mchezaji hata mmoja kama ambavyo imezoeeleka.

Kandanda safi na la kuvutia kutoka kwa wachezaji wa timu zote mbili zilitosha mchezo huo kumaliza dakika 45 za kwanza bila ya goli.

Kipindi cha pili kilianza kwa Kasi na kila timu ikisoma mchezo wa mpinzani wake ambapo kulisababisha kuwepo na mabadiliko ya wachezaji kwa kila timu kulingana na mipango ya walimu.Hata hivyo Kagera waliamua kumuingiza Hamis Kiiza ambaye leo amecheza kwa mara ya kwanza baada ya kusajiliwa Katika dirisha dogo.

Hamis Kiiza kuingia kwake kulikwenda kuleta mabadiliko kwa timu ya  Kagera ambayo iliamua kushambulia kwa kushutukiza kwa kuhakikisha mipira inayoanzia nyuma inafika kwa wachezaji waliokuwa wanashambulia lango la Simba 

Mbinu hiyo ilitosha kuifanya Kagera kuibuka na ushindi baada ya Hamis Kiiza kupokea pasi na Kisha kufanikiwa kupiga Mpira ambao uliingia golini baada ya kipa wa Simba Aishi Manula kushindwa kuuduka.
.
Hivyo hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika Kagera wameibuka na ushindi huo ambao umewafanya kupata alama tatu huku Simba wakiondoa bila ya kupata alama.Timu ya Simba Katika michezo miwili iliyocheza kabla ya kukutana na Kagera hawakuwa na matokeo mazuri kwani walipot na Mbeya City na kisha wakatoa sare dhidi ya timu ya MTIBWA 

Mwisho.
Previous articleKAMBI ZA HUDUMA ZA TIBA ZA KIBINGWA KATIKA MIKOA YA PEMBEZONI MWA NCHI KUWA ENDELEVU
Next articleMAHAKAMA KUU KANDA YA SONGEA YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA MFARANYAKI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here