Home LOCAL WAZIRI WA MAJI KUZINDUA MIRADI YA MAJI RUKWA

WAZIRI WA MAJI KUZINDUA MIRADI YA MAJI RUKWA

RUKWA.

Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso (Mb) anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili kwenye wilaya za Sumbawanga, Kalambo na Nkasi kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maji vijijini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana (15.12.2021) na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Denis Bandisa imesema Waziri Aweso ataanza ziara hiyo tarehe 17 na 18 mwezi huu ambapo atazindua miradi miwili ya maji kijiji cha Kizungu, Sopa na Kitete wilaya ya Kalambo.

Katika siku ya pili ya ziara yake atakagua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maji ya kijiji cha Kirando na Kisura wilaya ya Nkasi.

Pamoja na shughuli zingine Waziri Aweso atapata fursa ya kuongeza na wananchi kwenye maeneo yote ya miradi wakati wa ziara yake mkoani Rukwa.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Rukwa Mhandisi Pius Boaz alisema maandalizi ya ziara hiyo yamekamilika na kuwa wananchi wajitokeze kwenye maeneo ya miradi ili wamsikilize Waziri atakapozindua miradi na kuongeza na wananchi.

Mwisho.

Imeandaliwa na;

Afisa Habari Mkuu,

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

SUMBAWANGA

16 Desemba, 2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here