Home SPORTS TAIFA CUP ‘NETBALL’ YASHIKA KASI DAR

TAIFA CUP ‘NETBALL’ YASHIKA KASI DAR

 

Na: Stella kessy, DAR ES SALAAM

MASHINDANO ya Taifa (Taifa Cup) yamezidi kushika Kasi kwa michezo ya netiboli na soka kuonyeshana ubabe katika michezo hayo.

Mashindano hayo yanaendelea kutimua vumbi kwenye Viwanja mbalimbali vya Da es Salaam yakishirikisha timu kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

Katika matokeo ya juzi netiboli Kigoma imekubali kichapo cha magoli 47_23 dhidi ya Mbeya,huku Songwe waliibuka na ushindi wa magoli 47_22 dhidi ya Arusha,wakati Kaskazini Pemba walikubali kichapo cha magoli 447_23 dhidi ya Dodoma.

Matokeo mengine Pwani ikishinda magoli 36_35 dhidi ya Mwanza,Geita ikiikaanga magoli 45_14 dhidi ya Njombe,wakati mjini Magharibi ikiangusha kipigo cha magoli 58_29 dhidi ya Tanga,ikimaliziwa mtanange Kati ya katavi kukubali kichapo cha magoli 27_11 dhidi ya Tabora.

Kwa upande wa matokeo ya  soka wanawake Dar Es Salaam iliibuka na ushindi wa mabao 3_1 dhidi ya Tanga ,huku Kaskazini Unguja walishindwa kutambiana na Kigoma na kutoka sare ya 2_2 ,wakati upande wa wanaume Mara iliwaadhibu mabao 3_0 dhidi ya Rukwa katika michezo yao iliyochezwa kwenye Viwanja mbalimbali jijini Dar Es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here