Home SPORTS SIMBA IKO IMARA KUNYAKUA POINTI 3 DHIDI YA KMC KESHO

SIMBA IKO IMARA KUNYAKUA POINTI 3 DHIDI YA KMC KESHO

NA:  STELLA KESSY

MENEJA  wa timu ya Simba Patrick Rweyemamu amesema kikosi kipo tayari kupambania alama tatu dhidi ya ya KMC katika mchezo wa ligi kuu ya NBC utakaopigwa  ijumaa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi majira ya saa 10:00.

Rweyemamu amesema kikosi cha wachezaji 24 kilichosafiri Mkoani Tabora kipo vizuri na wapo tayari kwa mchezk ambao wanaamini utakuwa mgumu lkn watapambana kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

“Kikosi kimesafiri salama tabora wachezaji wako vizuri na jioni watafanya mazoezi ya kuweka sawa miili kutokana na uchovu wa safari” amesema.

“Tumekuja na wachezaji 24 na watu 14 benchi la ufundi tayra kwa mchezo tunajua mchezo utakuwa mgumu sisi ni mabingwa watetezi kwa hiyo tumejipanga kuhakikisha tunashinda “amesema Rweyemamu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here