NA: MWANDISHI WETU
Mwanamitindo chipukizi Kenny Abraham ‘Kenny_ kaiser75’, amewashukuru wadau wa mitindo na mashabiki zake kwa kumpigia kura zilizofanya kuwa mshindi wa Mwanamitindo bora chipukizi wa mwaka huu.
Tuzo hizo zimetolew a mwishoni mwa wiki iliyopita katika tamasha la mavazi la Bantu lilifanyika Morogoro eneo la Mto Mawe.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema anashukuru wadau kwa kumuona tuzo hiyo ni hatua kubwa kwake katika tasnia ya mitindo.
“Nimepata moyo wa kuongeza bidii katika tasnia ya mitindo nimeingia kwa muda mfupi ila wadau wameona nastahili kupata tuzo hii nawashukuru na ahidi kufanya vizuri zaidi ya hapa,” anasema
Alitoa wito kwa wanamitindo wenzake kujituma zaidi kuifanya kazi yao kua ajira kama zilivyo zengine kwa kua tasnia ya mitindo inakua kwa kasi hususa nchin kwetu Tanzania.