MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ,ametuwa ndoo kichwani mama kwa kuisaidia Serikali kapeleka maji Wilayani Kisarawe
Meya Kumbilamoto amepeleka maji kijiji cha Kauzeni kibuta Wilayani Kisarawe , kwa kuchimba kisima cha maji safi na salama ambacho kinawahudumia wananchi wa eneo hilo ambao walikuwa wakiangaika kichwani kusaka maji kwa umbali mrefu.
Kisima hicho kimezinduliwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano Selemani Jaffo Kata ya Kibuta kauzeni Wilayani Kisarawe mkoa Pwani thamani ya shilingi milioni 10 kisima kina urefu wa kina cha mita 120.
“Nimeunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kumtua ndoo Mama kichwani nimechimba kisima hichi kikubwa kwa gharama zangu ili kiwasaidie jamii ya eneo hili ambalo lina changamoto ya maji safi na Salama” alisema Kumbilamoto.
Meya Kumbilamoto alisema yeye ni mtu wa Jamii amesogeza maji karibu na wananchi kwa nia njema sio kuja kugombea Ubunge Kisarawe na mtu yoyote anarusiwa kusaidia Serikali
Meya alisema maji hayo yatawanufaisha wakazi wa eneo hilo ikiwemo wazazi wake katika eneo hilo alilozaliwa ,alikuwa akiwaona Wazazi wake wakisaka maji. kwa umbali mrefu.
Alimpongeza Meneja Shirika la Umeme Kisarawe kaika juhudi za kufanikisha umeme kufika katika kisima hicho kikubwa kinachowahudumia wananchi 5000.
Waziri wa Nchi Muungano na wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jaffo ,alimpongeza Meya Kumbilamoto kwa juhudi zake hizo za kusaidia serikali kumtua ndoo mama kichwani
Waziri Jaffo alisema wilaya hiyo ya Kisarawe ni wilaya ya kwanza aina maji Mwanamama anaweza akatafuta maji siku tatu au kukaa foleni yakipatikana unaoga ndoo nusu ila kwasasa Kisarawe Mjini kero hiyo imemalizika ..
Aliwataka wadau wengine kuunga mkono juhudi za Kumbilamoto kuwekeza katika sekta ya maji kusogeza maji karibu na Jamii.
“Unapopewa dhamana itumie kwa maendeleo kusaidia jamii Meya Kumbilamoto amekuwa mkombozi katika wilaya ya Kisarawe “ alisema Jaffo
Naye Mufti wa Tanzania Abubakari bin Zuberi alisema maendeleo katika nchi hayapatikani bila maji ,Wanyama ,viumbe,mifugo wanadamu wapo hai kwa ajili ya maji .
Mufti Zuberi alitumia nafasi hiyo kuombea amani idumishwe katika nchi yetu ,ikiwemo Kuwaombea afya njema viongozi wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ,Waziri Selemani Jaffo na Meya Kumbilamoto.
MWISHO