Home LOCAL MEYA KUMBILAMOTO APELEKA MAJI WILAYA KISARAWE

MEYA KUMBILAMOTO APELEKA MAJI WILAYA KISARAWE



NA: HERI SHABAN(PWANI)

MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ,ametuwa ndoo kichwani mama kwa kuisaidia Serikali kapeleka maji Wilayani Kisarawe

Meya Kumbilamoto amepeleka maji  kijiji cha Kauzeni kibuta Wilayani Kisarawe   , kwa kuchimba kisima cha maji safi na salama ambacho kinawahudumia  wananchi wa eneo hilo ambao walikuwa wakiangaika kichwani kusaka maji kwa umbali mrefu.

Kisima hicho kimezinduliwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano Selemani Jaffo Kata ya Kibuta kauzeni Wilayani Kisarawe mkoa Pwani thamani ya shilingi milioni 10 kisima kina urefu wa kina cha mita 120.

“Nimeunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kumtua ndoo Mama kichwani nimechimba kisima hichi kikubwa kwa gharama zangu ili kiwasaidie jamii ya eneo hili ambalo lina changamoto ya maji safi na Salama” alisema Kumbilamoto.

Meya Kumbilamoto alisema yeye ni mtu wa Jamii amesogeza maji karibu na wananchi kwa nia njema sio kuja kugombea Ubunge Kisarawe na mtu yoyote anarusiwa kusaidia Serikali

Meya alisema maji hayo yatawanufaisha wakazi wa eneo hilo ikiwemo wazazi wake katika eneo hilo alilozaliwa ,alikuwa akiwaona Wazazi wake wakisaka maji. kwa umbali  mrefu.

Alimpongeza Meneja Shirika la Umeme Kisarawe kaika juhudi za kufanikisha umeme kufika katika kisima hicho kikubwa kinachowahudumia wananchi 5000.

Waziri wa Nchi Muungano na wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jaffo ,alimpongeza Meya Kumbilamoto kwa juhudi zake hizo za kusaidia serikali kumtua ndoo mama kichwani

Waziri Jaffo alisema wilaya hiyo ya Kisarawe ni wilaya ya kwanza aina maji Mwanamama anaweza akatafuta maji siku tatu au kukaa foleni yakipatikana unaoga ndoo nusu ila kwasasa Kisarawe Mjini kero hiyo imemalizika ..

Aliwataka wadau wengine kuunga mkono juhudi za Kumbilamoto kuwekeza katika sekta ya maji kusogeza maji karibu na Jamii.

“Unapopewa dhamana itumie kwa maendeleo kusaidia jamii Meya Kumbilamoto amekuwa mkombozi katika wilaya ya Kisarawe “ alisema Jaffo

Naye Mufti wa Tanzania Abubakari bin Zuberi alisema maendeleo katika nchi hayapatikani bila maji  ,Wanyama ,viumbe,mifugo wanadamu wapo hai kwa ajili ya maji .

Mufti Zuberi alitumia nafasi hiyo kuombea amani idumishwe katika nchi yetu ,ikiwemo Kuwaombea afya njema  viongozi wetu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ,Waziri Selemani Jaffo na Meya Kumbilamoto.

MWISHO

Previous articleHABARI MAGAZETI YA LEO J.NNE DISEMBA 7-2021
Next articleAJIUA KWA WAYA KISA KUTOTAJWA MISA YA SHUKRANI KANISANI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here