Home SPORTS KIDUNDA AMTAKA KATOMPA AJIPANGE DISEMBA 26

KIDUNDA AMTAKA KATOMPA AJIPANGE DISEMBA 26

 


Na:Stella kessy, DAR ES SALAAM.

BONDIA wa ngumi za kulipwa Seleman Kidunda ametuma salamu kwa mpinzani wake Eric Tshimanga Katompa na kumueleza kuwa yeye sio mtu wa mchezo na wala hatanii akimtaka ajiandae kabla ya kukutana naye.

Pambano hilo la kulipa kisasi, linatarajiwa kuwa na mapambano 10 ya utangulizi ambapo sita yatakuwa ya kimataifa lakini pia katika pambano hilo  la Ubingwa wa  dunia wa WBF itafanyika  Desemba 26 mwaka huu.

Kauli hiyo ameitoa leo kwa waandishi wa habari, Kidunda amesema anataka kuonesha ulimwengu na watanzania kuwa hakuna bondia anayeweza kuja kushinda ndani ya ardhi ya Tanzania.

Kidunda amesema, anataka kuwaonesha ladha watanzania na ushindi upo kikubwa ni sapoti kutoka kwa watanzania wote katika pambano hilo muhimu.

“Nimejiandaa vizuri, ushindi upo na kikubwa ni kusubiri siku ya pambano ifike na hatatoka na ushindi wowote,”

“Nia ya ushindi ipo na na nitampiga Kamtopa kwa namna yoyote, kwa staili yoyote hatatoka kikubwa ni sapoti kutoka kwa watanzania,” amesema

Kwa upande wa muandaaji wa pambano hilo kutoka Peaktime Media, Kapteni Selemani Semunyu amesema amesema pambano kati ya Kidunda na Katompa ni la ubingwa wa WBF, uzito wa Kg 76 na litakuwa la raundi 10.

Amesema, pambano hilo litakuwa la kulipa kisasi baada ya Katompa kumchapa Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ na kuondoka na Ubingwa.

Semunyu amesema, kabla ya pambano hilo kutakuwa na mapambano 10 ya utangulizi na sita yatakuwa ya kimataifa  na litafanyika kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza.

“Nawashukuru sana wadhamini wote pia mnadhimu Mkuu wa Jeshi kwa kulisimamia pambano hili kuanzia mwanzo hadi mwisho na kusema ukweli bila yeye pambano hili lilikua na hatihatu ya kufanyika,”

“Ameahidi pia kama namba moja atashindwa kufika siku hiyo basi yeye anaweza kumuwakilisha na kuwa mgeni rasmi siku hiyo,” amesema

Mabondia wengine watakaopambana siku hiyo ni Ismai Galiatano dhidi ya Denis Mwale, Ibrahim Class vs Israel Kamwamba, George Bonalacha vs Hassan Milanzi, Pali Magesta vs Oscar Richard na Viguli Shafii vs Ally Kilongola.

Wengine ni Hamis Kibodi vs Iddy Jumanne, Grace Mwakamela vs Ruth Chisale, Najma Isike vs Leila Zayidu na Daniel Materu vs Haruna Swanga

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here